Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Habari mpya kuhusu Rufaa ya ubunge wa Mnyika: Hawa Ng’umbi Aomba Kesi Iondolewe Bila Gharama

Hawa Ng’humbi kupitia kwa wakili wake ameomba rufaa iondolewe mahakamani bila gharama. Ilikuwa ni baada ya maombi aliyotoa mapema kwa Wakili wa mujibu rufani, John Mnyika kwamba aruhuhusiwe kuondoa kesi hiyo na asamehewe gharama za kesi hatua ya rufaa. Afisa Habari wa Chadema ameeleza haya mapema leo asubuhi

Picha ya maktaba kupitia mitandao ya internet, Hawa Ng’umbi katikati na John Mnyika kushoto

Awali, mgombea huyo wa CCM Jimbo la Ubungo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, alikata rufaa tarehe 13/06/2012 kupinga uamuzi wa Mahakama ilioompa ushindi bwana John Mnyika mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu.

Hawa Ng'umbi alikata rufaa hiyo kwa madai kuwa hakuridhishwa na hukumu iliyompa ushindi Mh J.J.Mnyika

Hawa Ng,umbi alisema John Mnyika aliingiza laptop zake kwenye chumba cha kuhesabia kura ili zitumike kufanyia majumuisho ya kura na kudai kuwa lap top hizo zilimuongezea kura Mnyika. Pia alidai kuwa Mnyika aliingiza watu 5 kwenye chumba cha kuhesabia kura kinyume na taratibu za uchaguzi na akasisitiza kuwa Mnyika alimkashifu kwa kumwita fisadi kwenye vikao vya Halmashauri kwa kudai kuwa yeye ameuza nyumba ya serikali..kwa maana hiyo alilenga kumchafua ili akose sifa kwa wapiga kura wa Ubungo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO