Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: UGANDA WALIVYOTWAA UBINGWA WA CECAFA MARA YA PILI MFULULIZO; ZANZIBAR WALIVYOIADHIRI TANZANIA BARA KAMPALA JANA

Nahodha wa Uganda, Hassan Wasswa akiwa amenyanyua Kombe la Ubingwa wa CECAFA Tusker Challenge 2012 baada ya kuifunga Kenya kwenye Uwanja wa Mandela mjini Kampala, Uganda usiku wa kuamkia leo mabao 2-1 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo.

Wachezaji wa Uganda wakishangilia kutwaa Kombe la Ubingwa wa CECAFA Tusker Challenge 2012 baada ya kuifunga Kenya kwenye Uwanja wa Mandela mjini Kampala, Uganda usiku wa leo mabao 2-1 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo.

Robert ssentongo akimtoka Mieno

Hassan Wasswa akuwatoka wachezaji wa Kenya

Mshambuliaji wa Bara, John Bocco akiwatoka mabeki wa Zanzibar katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole Kampala leo. Zanzibar ilishinda kwa penalti 6-5, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90,  Bara wakitangulia kupata bao kupitia kwa Mwinyi Kazimoto dakika ya 10 kabla ya Abdallah Othman Ali kuisawazishia Zanzibar dakika ya 85.

Beki wa Zanzibar, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akimdhibiti mshambuliaji wa Zanzibar, John Bocco

Kiungo wa Bara, Athumani Iddi ‘Chuji’ akimtoka beki wa Zanzibar, Sabri Ally Makame

Kocha Mkuu wa Zanzibar, Salum Nassor Bausi akiwa amebebwa na wachezaji wake kwa furaha

Wachezaji wa Zanzibar wakishangilia baada ya mechi

PICHA ZOTE NA BIN ZUBEIRY BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO