TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' na ile ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' sasa zitakutana katika mechi ya kusaka mshindi tatu wa michuano ya kombe la Chalenji inayofikia tamati kesho nchini Uganda kwa kuzikutanisha katika hauta ya fainali Kenya na Uganda ambae ni mwenyeji wa michuano hiyo na bingwa mtetezi.
Timu hizo zitakutana katika mchezo huo leo baada ya jana kufungwa katika michezo yao ya nusu fainali ambapo Zanzibar Heroes ilitolewa kwa matuta na Kenya baada dakika 120 kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, huku Kilimanjaro Stars ikifungwa na Uganda mabao 3-0 yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji Emmanuel Okwi na Robert Snetongo.
Wachezaji wa Bara wakijadiliana baada ya kufungwa na Uganda katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge usiku wa leo kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala, Uganda. Uganda walishinda 3-0 na kutinga fainali, ambako watamenyana na Kenya kesho
SURA ZA HUZUNI; Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe kulia akifuatilia mchezo kati ya Bara na Uganda. Kushoto wake ni Waandishi wa Habari wa Tanzania, Somoe Ng'itu juu na Zaituni Kibwana pembe ni kabisa Z.H.
Cheki ulinzi huo langoni mwa Uganda, Ngassa na Bocco peke yao wangefanya nini
Amri Kiemba anakokota ngoma
John Bocco akiwa amezibiwa njia
John Bocco leo aliwekewa ulinzi mkali, kama unavyona hapa
Mrisho Ngassa akidhibitiwa na beki wa Uganda
Mwinyi Kazimoto akijaribu kufumua shuti mbele ya beki wa Uganda
Kipa kadaka, Ngassa na Bocco leo hoi
Kocha wa Stars, Kim Poulsen baada ya mechi
Kapteni Kaseja haamini macho yake
Emmanuel Okwi akifuatilia mchezo benchi baada ya kuumia na kutoka
Bocco mawindoni, lakini ulinzi wa kutosha ulimynima mabao leo
MATUKIO YA MAPAMBANO BAINA YA KENYA NA ZANZIBAR HEROES
Beki wa Zanzibar, Aggrey Morris akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili kwa penalti, Uwanja wa Mandela, Namboole katika Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge usiku wa leo. Zanzibar ilifungwa kwa penalti 4-2 na sasa itamenyana na Bara katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Jumamosi.
Khamis Mcha 'Vialli' akishangilia baada ya kuifungia Zanzibar bao la kwanza
Adeyom Saleh Ahmed akimtoka beki wa Kenya, Joackins Atudo
Nadir Cannavaro ameruka na kipa wa Kenya
Mcha anapasua ukuta wa Kenya
Mcha Vialli kamlamba mtu chenga, kamuacha chini anaambaa
Suleiman Kassim 'Selembe' akipasua katikati ya msitu wa wachezaji wa Kenya
Kocha wa makipa wa Zanzibar, Farouk Ramadhan akimpa maelekezo kabla ya mechi kipa Mwadini Ally
Kikosi cha Zanzibar
Kikosi cha Kenya
Wachezaji wa Zanzibar wakiwa wametahayari baada ya kufungwa bao la pili la kusawazisha
Mike Barasa wa pili kutoka kulia akishangilia bao lake la pili
Zanzibar wakisujudu baada ya kufunga bao la kwanza
Kipa kaenda kulia, penalti ya Aggrey imetinga kushoto
Aggrey akiwaongoza wenzake baada ya kufunga bao la pili
Jaku Juma akipambana
Adeyom akimtoka beki wa Kenya
Adeyom anajaribu
Jaku Juma akipambana
Aggrey ameruka na mtu
PICHA ZOTE NA BIN ZUBEIRY BLOG
0 maoni:
Post a Comment