Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

STARS YATINGA ROBO FAINALI BAADA YA KUIANGUSHIA MVUA YA MAGOLI SOMALIA 7-0; NGASSA ATUPIA 5

 

 

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala

TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars imefuzu kuingia Robo Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge, baada ya kuilaza Burundi mabao 7-0 katika mchezo uliofanyikakwenye Uwanja wa Lugogo mjini hapa.

Matokeo hayo yanaifanya Bara itimize pointi sita baada ya kucheza mechi tatu na sasa, wakishinda mbili na kufungwa moja.

Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo ilionyesha kandanda safi na kusisimua mashabiki wa Tanzania waliokuja kuoiunga mkono hapa, akiwemo Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Alhaj Juma Nkamia.

Iliwachukua sekunde 48 tu Stars kupata bao la kwanza, kupitia kwa mshambuliaji wa Simba SC, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premum Lager pia, Mrisho Khlfan Ngassa aliyewazidi ujanja mabeki wa Somalia.

Kabla hawajakaa vizuri, Somalia walipachikwa bao la pili, dakika ya 23 lililofungwa na Ngassa tena, aliyeunganisha kona nzuri ya Issa na Rashid.

John Bocco ‘Adebayor’ alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo na la tatu kwake katika mashindano haya dakika ya 26 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Issa Rashid kutoka wingi ya kushoto.

Bocco tena aliwainua vitini mashabiki wa Tanzania kwa kufunga bao la nne kwa kichwa, akiunganisha krosi ya Ngassa dakika ya 41.

Ngassa alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo dakika ya 44 na la tano kwa Stars baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Hussein Abdallah kufuatia shuti kali la Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’

Somalia ilipata pigo dakika ya 30, baada ya kipa wake namba moja, Mohamed Abdullah kuumia baada ya kugongana na Bocco na kutoka, nafasi yake ikichukuliwa na Hussein Abdallah. 

Kipindi cha pili Stars walirejea na moto wao na tena na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi yaliyotiwa kimiani na Ngassa yote dakika za 73 pasi ya Erasto Nyoni na 74 pasi ya Ramadhani Sinago ‘Messi’.

Kwa kufunga mabao matano, Ngassa sasa ameingia kwenye mbio za kaiti cha dhahabu akikwa anaongoza, akifuatiwa na Bocco ambaye ana manne hivi sasa.

Kocha wa Stars, Mdenmark Kim Pouslen baada ya mchezo huo, alisema aliwapongeza vijana wake kwamba wamejitahidi kucheza vizuri na akasifu pia hali nzuri ya Uwanja wa Lugogo kuwa ilichangia ushindi huo.

Mbunge Nkamia alisema kwamba amevutiwa na soka ya vijana leo na anaamini wana uwezo wa kurejea na Kombe nyumbani. Nkamia aliwapongeza wadhamini wa Stars kwa kuchangia mafanikio ya timu hiyo tangu waanze kuidhamini na akaomba Watanzania zaidi wajitokeze mjini hapa kuisapiti timu hiyo.

Waandishi wa Habari waliopo mjini hapa pia wamevutiwa mno na kiwango cha timu hiyo na kusema wana wana imani itafika mbali.

Wallace Karia, Mjume wa Kamati ya Utendaji ya TFF aliye hapa Uganda amesema amefurahishwa na kiwango cha timu na anaamini itafika mbali.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa Kilimanjaro Stars, George Kavishe ametuma salamu za pongezi kwa ushindi wa leo na mafanikio ya kutinga Robo Fainali na kusema anatakia mafanikio zaidi timu hiyo.

Katika mchezo wa leo, kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Kevin Yondan/Ramadhani Singano, Shaaban Nditi, Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco/Christopher Edrwad, Frank Domayo/Athumani Iddi na Amri Kiemba.

Somalia; Mohalim Abdullahi/Hussein Abdallah dk30, Ali Mohamed, Said Mahamud, Ali Dadir, Sadaq Abdikadir, Mohamed Salah, Abdikarim Abubakar, Abdallah Mohamed/Hamza Mukhtar, Ahmed Abdikadir Dahir/Muhad Hajji na Ali Ahmed Ali.  

Katika mchezo mwingine uliopigwa kwenye Uwanja wa Nankurunkuru, Burundi ilishinda 1-0 bao hivyo kuongoza Kundi B baada ya kufikisha pointi tisa.

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakisalimiana na wachezaji wa Somalia kabla ya mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda

Mrisho Ngassa akipongezwa na Athuman Idd baada ya kufunga goli la kwanza

Mrisho Ngasa wa Kilimanjaro Stars mwenye mpira akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Somalia wakati wa mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda

Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichopambana na timu ay Somalia katika mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda

Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars Mrisho Ngassa akiambaa na mpira uliozaa goli la kwanza sekunde ya 48

Mrisho Ngassa akishangilia moja ya goli kati ya matano aliyofunga wakati wa mchezo na Somalia uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda

Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, John Bocco (kulia) akimtoka beki wa timu ya Somalia, Abdallah Mohamed

Boko akishangilia moja ya goli wakati wa mchezo na Somalia

Mashabiki wa Kilimanjaro Stars waishio nchini Uganda wakati wa mchezo wa Cecafa Challenge dhidi ya timu ya Somalia uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda

Mrisho na mpira wake baada ya kufunga mabao matano

PICHA ZOTE NA SHAFFIH DAUDA.COM

seria signature

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO