Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Besidei za Club Bilicanas kutimiza miaka 20, na Clouds Fm miaka 13

***********

WADAU  mbalimbali  wa burudani  usiku  wa kuamkia jana walifurahia kwa pamoja  na kula keki ya miaka 20 ya klabu ya Kimataifa ya Bilicanas na miaka 13, ya Clouds Fm,  iliyoambatana na shamrashamra mbalimbali ndani  na nje ya  ukumbi huo.

Sherehe hizo ziliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group, Dk. Lilian Mtei  ambapo aliwashukuru wadau hao kwa kuwa bega kwa bega na klabu hiyo, tangu 1992. “Tunawashukuru sana kwa kuwa nanyi mara zote inatia faraja kwetu na tutaendelea kutoa huduma bora siku zote|” alisema Mbowe.

Mtei pia aliwashukuru wafanyakazi mbalimbali waliofanikisha ukumbi huo kufikia hapo na kutoa heshima ya kipekee kwa wafanyakazi  waliokuwapo  tokea inaanza hadi ilipofikia miaka 20 na hatimaye  kukata keki hiyo.

“Uwepo wa miaka 20, tuna kila sababu ya kuwapongeza wafanyakazi  tuliokuwa nao toka mwanzo hadi leo, na kwa heshima ya pekee  Mama Victor na Mrs Mitemo  ndiyo watakao kata keki hii” alisema Mtei.

Keki hiyo ilikatwa na wafanyakazi   hao  Monica  Victor   na Pili Mitemo  ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni marehemu.

Aidha, kwa upande  Clouds FM, iliwakilishwa na Wasiwasi Mwabulambo ambaye alipongeza klabu Bilicanas kwa kuwa mstari wa mbele katika kuinua sanaa nchini hasa kwa kuwasaidia wasaidia wasanii kufikia malengo yao.

Kwa upande wake  Ibrahim Tuwa ‘Dj Ibra’ aliyekuwa akisherehesha  shughuli hiyo, aliwaomba wadau kuendelea kuwaunga mkono na wataendelea na huduma bora zaidi ha hapo. Dj Ibra alijiunga na Bilicanas tokea 2002,ambapo mpaka sasa ana miaka 10 kwenye klabu hiyo  iliyowahi kuwa na madj maarufu waliopita  hapo ambao wengi wao wapo kwenye vituo vya televisheni na redio.

Bendi ya muziki ya dansi ya Sky Light ikitumbuiza katika sherehe za kutimiza miaka 20 ya Club Bilicanas na miaka 13 ya Clouds FM. (Picha zote na Habari Mseto Blog)

Sherehe hizo zilipambwa na shamrashamra za aina mbalimabli ikiwemo kukati keki pamoja na kufungua shampeni

Dk. Lilian Mtei akizungumza katika hafla hiyo.

Mwakilishi wa Clouds FM, Wasiwasi Mwabulambo akizungumza katika hafla hiyo

Tukate keki

Mmoja kati ya wafanyakazi wa kwanza wakati Bilicanas Club inaanzishwa miaka 20 iliyopita, Monika Victor akimlisha keki, Dk. Lilian Mtei wakati wa hafla ya kutimiza miaka 20 ya klabu hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Maandalizi ya keki

Pili Mitemo ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni marehemu akipokea keki kutoka kwa Dk. Lilian Mbowe kwa ajili ya kuwapa wadau waliojitokeza katika hafla hiyo

Mzee Ali Ramadhan Mkude nae akuwa mbali katika mnuso wa Bilicanas Club kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa

Mdau Bi. Agnes Mbowe akillishwa kipande cha keki na Dk. Lilian Mtei.

DJ Ibrahim Tuwa 'Dj Ibra' akilishwa keki wakati wa hafla hiyo

Dk. Lilian Mtei akimlisha kipande cha keki Meneja Msaidizi wa Vinywaji wa Club Bilicanas, Amandus Agant wakati wa Birthday ya Bilicanas Club kutimiza miaka 20.

Monica Victor akigawa keki kwa wadau waliofika katika sherehe hizo.

Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akiwa na mmiliki wa blog ya Bongoweekend, Khadija Kalili pamoja na wadau wengine. 

Watu wa mataifa mbalimbali wakicheza muziki katika ukumbi wa Bilicanas. 

Stori Na Andrew Chale, Picha kwa hisani ya Kamanda wa Matukio – Richard Mwaikenda

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO