Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MKE WA FILBERT BAYI AMFUATILIA MWANARIADHA MAARUFU WILHELM GIDABUDAY JIJINI ARUSHA

MWANARIADHA Willhelm Gidabuday (pichani) ameelezea mshangao wake kwa kitendo cha Mke wa Filbert Bayi kumfuatilia kiukachero hadi maneo anayofanyia shughuli zake Jijini Arusha.

Gidabuday au Gida kama wengi wanavyomuita amesimulia mkasa huo mapema asubuhi ya leo na kueleza kuwa akiwa anaongozana na mwenzake Gorath Jonh na mtu mwingine aliyemtambulisha kwa jina moja la Mzee Wade wa Arusha, alikutana na Mama Bayi  akiwa na gari la Francis John aliyekuwa Rais wa chama cha riadha (RT), gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na mtu aliyemtambulisha kama Gerald Solomoni babu.

Gida anasimulia zaidi kuwa katik gari hilo Mama Bayi alikuwa amekaa siti ya bairia pamoja na Fabian Joseph aliyekuwa siti za nyuma na kwamba baada ya kuwafikia karibu Mama Bayi alimsemesha maneno ambayo yaliashiria hasira ama shari fulani dhidi yake.

Kwa mujibu wa maelezo ya Gida sehemu ya mazungumzo yao ilikuwa hivi..
MAMA BAYI: Gida vipi,
MIMI: Safi shikamoo mama,
MAMA BAYI: Malapa yako sasa utayasemea wapi?,
MIMI: Mungu anajua,
MAMA BAYI: Wewe una Mungu?,
MIMI: Mungu yupo; Heri ya mwaka mpya,
MAMA BAYI: Kwako mwaka mpya umefika?

Haya yalitokea leo asubuhi mitaa ya mzunguko wa mnara wa Mwenge, jirani na jengo la kumbukumbu ya Azimio la Arusha.

Mbali na hayo Gidabuday alifanya mahojiano na blog ya Wazalendo 25 na kueleza kuwa  ana mikakati mikubwa sana hapa nchini ya kuinua mchezo wa riadha kutoka ngazi ya chini hadi Kimataifa. Pia amesema baada ya Sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya anatarajia kufanya jambo moja la kihistoria ambalo hata TOC hawaja wahi kulifanya, na kudai kuwa ni mapema mno kuliweka wazi.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO