Pichani kulia ni John Bayo aliyewahi kuwa Diwani Kata ya Elerai Jijini Arusha kupitia Chadema wakati huo kabla ya kuvuliwa uanachama yeye na wenzake wanne kwa makosa ya utovu wa nidhamu kwenye chama hicho; anaonekana kukabidhiwa kadi ya uanachama wa CUF na Mwenyekiti Prof Ibrahim Lipumba.
Taarifa ambazo Blog hii imezipata na kuthibitisha zinaeleza kuwa John Bayo ambae kwa sasa ni mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) anatakiwa kukamatwa kwa amri ya Mahakama kwa kushindwa kulipa Sh 1,511,650/= kwa Chadema kufuatia yeye na wenzake kushindwa katika shauri walilofungua kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema na Kamati Kuu ya chama hicho zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Hati hiyo ya kukamatwa kwa John Bayo (Civil case No 56 Warrant of arrest in execution order 21, rule 36..) imetolewa juzi na Hakimu Chalz Magesa, ambae anakumbukwa kuwahi kuandika hati nyingine ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Freeman Mbowe na kufikishwa katika Mahakama hiyo.
Fedha ambazo Bayo ameshindwa kulipa ni sehemu ya malipo awamu ya kwaza kwa kila mtu kama ilivyoamriwa na Mahakama kwamba baada ya kushindwa kesi walipaswa kuilipa Chadema jumla ya Sh Milioni 15 ambazo zilipaswa kulipwa kwa wamu mbili kwa mgawanyo sawa kwa kila mmoja.Nusu ya kwanza (mil 7.5) ilipaswa kulipwa mara tu baada ya hukumu na kiasi kilichobaki kilipwe katika muda wa miezi miwili baada ya siku ya hukumu.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa watu wengine waliokuwa madiwani wa Chadema kabla ya kuvuliwa uanachama, ambao nao wameshindwa katika kesi hiyo; Rehema Mohamed, Charlz Mpanda, Estomih Mallah na Rubeni Ngowi wamekwishalipa kisi kama hicho hicho. Baadhi walipata ufadhili wa mwanachama wa CCM kuwalipia madeni hayo.
Awali kesi hiyo ya kupinga kuvuliwa uanachama ilitokana na madiwani hao kufungua kesi ya kupinga kufukuzwa na kuvuliwa uanachama baada ya kudaiwa kukiuka sheria na kanuni za chama, zikiwemo makubaliano ya kutomtambua Meya wa Arusha Gaudence Lyimo wa Chama cha Mapinduzi(CCM) ambae CHADEMA wanadai hakupatikana kwa njia halali kisheria.
Waliokuwa madiwani wa Chadema kabla ya kuvuliwa uanachama katika picha ya pamoja walipoitwa Dodoma kuhojiwa na Kamati Kuu ya Chadema mwaka jana.
0 maoni:
Post a Comment