Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Rais wa Zamani wa Madagaska Marc Ravalomanana Amekubari Kurudi Nchini Kwake Kutoka Uhamishoni

Na: Veronica Kazimoto – MAELEZO

Dar es Salaam

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amefanikiwa kufanya mazungumzo na Rais wa zamani wa Madagaska Marc Ravalomanana ambaye amekubari kurudi nchini kwake baada ya kuwa uhamishoni nchini Afrika Kusini tangu mwaka 2009.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Raisi Kikwete amesema Ravalomanana amekubali pia kutokugombea katika uchanguzi utakaofanyika nchini humo mwezi Mei 2013 ili kuleta amani na utulivu.

“Nimezungumza na Rais Ravalomanana na amekubali kurudi nchini kwake madagaska na kukubali kutokukugombea uchaguzi ujao kama maamuzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yalivyofikiwa katika vikao vyake vya hivi karibuni”, amesisitiza Rais Kikwete.

Raisi kikwete amefafanua kuwa Ravalomanana anarudi nchini Madagaska bila masharti yoyote na atapewa ulizi na Serikali ya nchi hiyo ikisaidiana na Jumuiya ya SADC.

Kwa upande wake Rais Ravalomanana amemshukuru Rais kikwete kwa kufanikisha mazungumzo hayo na amesema anaheshimu maamuzi yaliyotolewa na SADC kwa lengo la kuisaidia Madagaska kuwa katika hali ya amani.

“Ninamshukuru Rais Kikwete kwa kufanikisha mazungumzo haya na niko tayari kurudi nchini kwangu kujenga, kuimarisha na kushirikiana na wananachi ili kuleta amani na utulivu,” amesema Ravalomanana.

Rais kikwete alipewa jukumu na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika la kufanya mazungumzo na Marais wote wa wawili, Rais wa sasa wa Madagaska Andry Rajoelina na Rais wa zamani Marc Ravalomanana ambapo mazungumzo bado yanaendelea kwa upande wa Rais Rajoelina.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO