Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TIMU YA WABUNGE WA TZ ILIVYOWABANJUA WENZAO KENYA 51-25

Timu ya Tanzania

Tanzania yaendeleza ubabe wa kwa timu za mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya timu ya mpira wa kikapu wananwake kuinyanyasa Kenya Bunge Sports Club kwa mabao 51-25. Wakati huohuo, timu ya wanaume imeedelea kutoa adhabu kali leo ikiwa ni zamu ya Rwanda ambapo hadi kipenga cha mwisho Tanzania 6 Rwanda 0. Jana Kenya ilibamizwa bao 5-0

Timu ya Kenya

Tanzania Bunge Sc

Tanzania Bunge Sports Club Football imefanya maajabu katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi jana kwa kuwabamizwa wenyeji wao timu ya Kenya Bunge Sports Club Football mabao 5-0e katika michezo ya mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Nairobi. Mashindano hayo yaliyofunguliwa rasmi juzi tarehe 7 Disemba na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margreth Natongo 

Katika mashindano haya ambayo hufanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Waratibu wa michezo hii ni Jumuiya pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu Burundi haikushiriki.Chini ya ukufunzi wa Naibu Waziri (TAMISEMI) Mhe. Kasim Majaliwa (Mb) .na uongozi wa Mhe. Idd Azzan (Mb) mabao hayo yalifungwa na Mhe Amos Makala (Mb), Yusuf Soka (2), Mark Tanda na Mhe. Joshua Nassari. (Na Prosper Minja)

Taarifa hii ilichapichwa na DINA ISMAIL BOG juzi 10 Desemba 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO