Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SHEREHE YA TAWI LA CHADEMA- DMV YA KUUAGA MWAKA 2012 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2013 M4C

Viongozi wa Tawi la CHADEMA DMV walipokuwa katika sherehe ya kuuaga mwaka 2012 na kukaribisha mwaka mpya 2013 M4C imefana sana, siku ya Jumamosi Desemba 22, 2012  katika ukumbi wa Mirage Hall iliokuwepo maeneo ya Hyattsville Maryland nchini Marekani.

Viongozi wa CHADEMA DMV waliweza kukamilisha  yale walioyapanga katika mkutano mzima ulioandaliwa na tawi hilo la CHADEMA ndani ya uongozi  mpya uliochaguliwa na wana-DMV kwa upande wa Chama hicho ambao  siku ya Jumamosi ya Desemba 22,  baadhi ya viongozi hao waliongea mambo muhimu kuhusu maendeleo ya chama hicho pamoja na mustakabali mzima  wa yanaoendelea nchini Tanzania.

 

Mhe. Baby Mgaza akiwa na amejiremba na mitindo ya M4C

 Kadi hii hapa..

Katibu mwenyekiti wa upande wa wanawake Mhe. Baby Mgaza wakati alizungumza na wana DMV

wadau

Utaifa mbele

Wazee pamoja na Uongozi mzima wa Tawi la CHADEMA-DMV wakiongea mustakabali wa mambo mbalimbali yanayoihusu Tanzania

Wanachama wa CHADEMA DMV wakiwa na baadhi ya wana DMV katika sherehe hiyo

Baadhi ya wana-DMV waliohudhuria ndani ya hafla hiyo ilioandaliwa na tawi la CHADEMA DMV

 Nasie tumo...Mmiliki wa  swahilivilla.blogspot.com (kofia nyekundu) aliyeleta taswira hizi na wadau

 Mkereketwa

Maktibu kwa upande wa wanawake Mhe. Baby Mgaza (kushoto), na Mwenyekiti wa wanawake Tawi la CHADEMA-DMV Mhe. Fatma Khamis.

Katibu wa Chadema DMV Mhe. Isdori Focus Lyamuya alitoa changamoto  za kukitakia chama chake maendeleo na ushirikiano mwema katika mpango mzima wa kuaga Mwaka 2012 na kukaribisha mwaka mpya 2013 M4C.

mwenezi wa CHADEMA Mhe. Hussein Kauzera maarufu kama DJ Rodgers akimwaga  sera na hotuba makini kuhusu sherehe ya kuuaga mwaka 2012 na kukaribisha mwaka mpya 2013 M4C

Mwenyekiti wa Tawi la Chama cha CHADEMA DMV Mhe. Cosmas Wambura, akiwahamasisha wana DMV kuhusu mipangilio ya Chama pamoja na kusisitiza mpango mzima wa kujiunga na tawi hilo liliopo Washington DC kwa nia njema ya kuitakia Tanzania mabadiliko ya M4C katika mwaka mpya wa 2013 ambao ni mategemeo makubwa ya kusonga mbele.

katibu wa uongozi uliopita Bwa. Liberatus Mwang'ombe a.k.a  Bagasa Libe pia aliongea mawili matatu 

 Wadau shereheni

Muongozaji na mshereheshaji katika hafla hiyo MC Jacob Merere akipata picha ya pamoja  kwenye sherehe ya kuaga mwaka 2012 na kukaribisha mwaka mpya 2013 M4C.

Baadhi ya ma CCM-DMV, Katibu Mwenezi, Benjamin Mwaipaja (wa pili kushoto) akiwa na Yasini Landi (wa kwanza kulia), kama kawaida yao washereheka kama Watanzania wanaojali Taifa lao!

Profesa Boaz (katikati) akiwa na Mhe. Atha pamoja na mkereketwa wa CHADEMA Bw. Emmanuel Muganda wakibadilishana jambo katika sherehe ya CHADEMA-DMV.

Mshereheshaji wa tukio zima la hafla hiyo MC Jacoub  akifanya vitu vyake. 

Mwenyekiti wa Wanawake Mhe. Maryam Khamis akiongea na wana DMV katika hafla hiyo. Chanzo: MICHUZI BLOG via WAZALENDO25 BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO