Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Bidhaa mpya za CHADEMA toka nje ya nchi zilizoingizwa sokoni zikiwa na nembo ya M4C… miamvuli, opena, key holder, nguo, mipira, suti, kofia n.k Ubora ni wa hali ya juu!

DSCN6591Miamvuli ya saizi tofauti. Blog hii iliweza kushuhudia wapenzi, marafiki na wanachama wa Chadema wakigombea kununua bidhaa hizi katika mjumuiko wa marafiki hao Jijini Arusha jana katika Hoteli ya Snow Crest. Mjumuiko huo uliandaliwa na kamati maalumu ya Chadema Arusha kwa nia ya kutengeneza mtandao wa kufanikisha usambazaji wa malengo ya M4C maeneo tofauti ya nchi. Kamati hiyo ilikabdihi kwa chama mkoa vifaa vya muziki wa jukwaani vyenye thamani ya jumla ya sh milioni 14 na kuahidi kuendelea na mchakato wa kutafuta gari la matangazo.

DSCN6413“opener” za vizibo vya soda au bia za chupa

DSCN6406bendera za ndani ya magari

DSCN6411“key holder” za aina tofauti, mpira wa miguu na miamvuli midogo

DSCN6407kofia za aina na saizi tofauti

DSCN6599t-shirt za rangi na aina tofauti

DSCN6594sehemu ya vazi la suti ya khaki

Mbali na bidhaa hizi chache pichani, ziko nyingine ndogo ndogo za kila aina na zinaelezwa kuwa ni ingizo maalumu kutoka nje ya nchi!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO