Mbunge wa wilaya ya Ilemela Highness Kiwia akihutubia wananchi waliofurika jana jioni kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza kwaajili ya kuwasilisha pingamizi la kumkataa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe kwa madai aliyoyatoa ya kutolitendea haki jimbo hilo.
Mbunge Ezekiel Wenje (CHADEMA) akihutubia. Wenje alishusha madongo kwa diwani wa Kata ya Kitangiri Henry Matata, ambaye sasa ndiye Meya wa Manispaa ya Ilemela (CHADEMA) akisema kuwa "Watu wa Kitangiri hawakumchagua Matata walichagua CHADEMA, sasa kwa kuwa alitokea CHADEMA, Matata akabebwa na upepo wa CHADEMA naye akajikuta yumo, Lakini watu wa Kitangiri kimsingi hawakumpigia kura Matata, waliipigia kura CHADEMA”
Katika kusanyiko hilo CHADEMA walipitisha karatasi kwa wananchi waliofika viwanjani hapo ili wasaini kuunga mkono hoja ya kumkataa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe na hizi ndizo karatasi za majina na sahihi zilizo kusanywa viwanjani hapo.
Mmoja kati ya wananchi akisaini karatasi kama mkazi wa ilemela viwanjani hapo kuunga mkono hoja ya kumkataa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe kutokana na sera zilizoainishwa jukwaani na wabunge hao.
Mbunge wa Ilemela Highness Kiwia ameanisha maeneo yaliyopelekea maamuzi hayo ya kumtaka Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda kumwondoa mkurugenzi huyo wa jiji kuwa ni pamoja na
1. Kuipa nguvu Halmashauri ya jiji la Mwanza kuendelea kusimamia ugawaji wa viwanja vipatavyo 3500 katika Manispaa ya Ilemela.
2. Uhamishaji wa soko la Mwaloni Kirumba kutoka katika ramani ya Ilemela kwenda Nyamagana.
Mbunge huyo amesema kuwa wakati wa kutoa matamko umepitwa na wakati sasa ni wakati wa vitendo hivyo ofisi yake imejipanga kuhakikisha kuwa ugawaji wa viwanja 3,500 vya Ilemela na soko la Mwaloni Kirumba kubaki kuwa mali ya Ilemela kutokana na vielelezo vya mipaka ya nchi na haki stahiki.
Mbunge wa Musoma mjini Bw. Makongoro naye alikuwepo.
Utulivu wa wananchi kusikiliza kinachojiri akili mkichwa kutafakari.
Hapa karatasi zilizosainiwa zikikusanywa na Red Brigade wa CHADEMA Mwanza ndani ya kusanyiko hilo kusaini kuunga mkono hoja iliyotolewa ya kumkataa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe kutokana na sera zilizoainishwa jukwaani na wabunge hao
Mwananchi akitafakari kabla ya kusaini....
Mwalimu Kamanzi (kushoto) akiwa ameketi na diwani wa kata ya Kirumba Mr. Kahungu mara baada ya kukabidhiwa madawati 10 na Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje (hayupo pichani) kama sehemu ya shukurani kwa watu wa wilaya ya Ilemela kushiriki vyema kuichangia wilaya ya Nyamagana katika harambee ya madawati kwa shule za msingi iliyofanyika mapema mwaka huu.
Aliyekuwa mwanachama wa CCM Thomas Pesanga Chacha (mwenye shati jeupe) akinyanyua juu kadi yake mpya aliyokabidhiwa na CHADEMA. Kwa mijibu wa maneno yake jukwaani amesema kuwa, amekuwa mwanachama wa CCM tangu mwaka 1980, akishikilia nyadhifa mbalimbali nafasi yake ya mwisho ni Ujumbe Kamati ya Utekelezaji Baraza la Wazazi Mkoa wa Mwanza aliyoitumikia tangu mwaka 2003 - 2008 kabla ya kutemwa kwenye uchaguzi uliofuata akisota benchi kukosa nyadhifa mbalimbali kwa takribani miaka 5 sasa licha ya kikipenda chama hicho na kukitumikia kwa moyo wote na sasa ameamua kuhamia CHADEMA.
PICHA ZOTE NA MAELEZO: G SENGO BLOG
0 maoni:
Post a Comment