Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HATIMAYE GAZETI LA MWAHALISI LAFUNGULIWA, KURUDI MTAANI WIKI IJAYO

HATIMAYE  Mahakama kuu imelifungua rasmi Gazeti la Mwanahalisi ambalo lilifungiwa na serikali kwa mda usiojulikana .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

       Akizungumza na Fullhabari.blogs, Mhariri wa Gazeti la Mwanahalisi ,Jabir Idrisa amethitisha kuwa Jaji wa mahakama kuu Salvatory Bongole,amelifungulia Gazeti hilo na kulitaka liendelee na kazi yake ya kuhabarisha umma  baada kubainika katika kulifungia kwake kanuni zilikiukwa.

        Amesema hukumu hiyo imetokana na kesi namba 27 ya mwaka 2013 ambapo Kampuni ya Hali halisi limited  ambao ni wachapishaji wa Gazeti la Mwanahalisi walikuwa wakitaka patio la hatua ya waziri wa Habari Fenera Mukangala juu ya kulifungia  Gazeti hilo, Katika kesi ambayo iliwakilisha kwa  Upande wa Serikali  na ofisi ya Mwanahseria mkuu  wa Serikali

Jabir amesema Mahakama imebaini waziri wa Habari hakufuata  sheria katika kulifungia gazeti hilo,licha ya kuwa na mamlaka ya kutokana na sheria ya Kandamizi ya  Magazeti ya mwaka 1976 inampa  uwezo wa kulifungia gazeti,

    Amesema Sheria iyo inamtaka waziri husika kufuata hatua kabla ya kulifungia Gazeti ambapo hatua hiyo ni kuwafuata wale anawaowatuhumu ili wapate utetezi na kuchukua hatua lakini waziri huyo alipolifungia Gazeti hilo  hakufuata hatua hizo.

   HATUA GANI INAFUATA BAADA YA HUKUMU HIYO.

Mwandishi huyo mwandamizi amesema kwa sasa kinachofuata ni kutaka fidia toka serikalini juu ya hasara iliyopatika wakati Gazeti hilo lilipokuwa limefungiwa huku akisema mahakama imeamulu wafanye hivyo.

      Amesema Chengine kinachofuata  ni mwenyewe Mmiliki wa Gazeti hilo akiamua kuchapisha Gazeti hilo  anachapisha  au aache kutokana na mahakama hiyo kumruhusu.

Kufunguliwa huko kwa Gazeti la kiuchunguzi la Mwanahalisi kunakuwa ni kama ushindi kwa Mkurugenzi wa Gazeti Saed Kubenea Mara kwa mara amekuwa ikidai serikali kulifungulia Gazeti hilo kimakosa.MWANANCHI

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO