Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Halmashauri ya Jiji la Tanga yashauriwa kuandaa Miradi inayoendana na Mahitaji ya Wananchi


Halmashauri ya Jiji la Tanga yashuriwa kuandaa  Miradi inayoendana na Mahitaji ya Wananchi
Na Adili Mhina, Tanga.
Halmashauri ya Jiji la Tanga imeshauriwa kuandaa miradi ya kupima na kuuza viwanja vinavyoendana na mahitaji halisi ya wananchi ili kuhakikisha viwanja hivyo vinanunuliwa kwa wakati na wananchi wanavitumia shughuli za maendeleo.

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati wa ziara ya timu ya ukaguzi wa maradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango katika mradi wa viwanja wa mji mpya wa Pongwe unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Jiji la Tanga na Kampuni ya Amboni Sisal Properties Limited.

Kiongozi huyo alitoa ushauri kufuatia kutoridhishwa na taarifa iliyotolewa na Afisa Mipango Miji wa jiji hilo, Bw. Joseph Mafuru kuwa mradi wa mji mpya wa Pongwe ulianza rasmi mwaka 2014 lakini hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana viwanja 510 tu kati ya viwanja 1000 ndivyo vilivyokuwa vimenunuliwa licha ya wanachi kufahamu uwepo wa mradi huo.

Kufuatia taarifa hiyo, Mwari aliamua kupitia ramani ya mradi na kubaini kuwa baadhi ya viwanja vilikuwa ni vidogo sana ikilinganishwa na mahitaji halisi ya wananchi. Vile vile baadhi ya maeneo ambayo yalionekana kuwa ni ya muhimu kwa ajili ya makazi na kwa fursa za biashara yalitengwa kwa ajili ya matumizi mengine kama maegesho ya magari.

“Inavyoonekana wanachi wengi hawajanunua viwanja hivi kwa kuwa ni vidogo sana, watu wanahitaji maeneo yenye nafasi, sio ukijenga nyumba tu kiwanja chote kimekwisha. Nimeona kuna maeneo ambayo yanapendwa sana kwa makazi na ni fursa kwa biashara lakini hapa mmeyatenga kwa ajili ya maegesho ya magari, vitu kama hivi vinasababisha wanachi wasivutiwe na maeneo yenu,” alieleza Mwanri.

Aliongeza kuwa mradi wa kupima na kuuza viwanja kwa wananchi ni kitu cha kutiliwa mkazo sana hususani katika maeneo ya mijini ambako kumekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa adhri na uwepo tatizo la makazi holela. Hivyo, ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha inatekeleza wajibu huo kikamilifu na viwanja vinauzwa kwa bei isiyowaumiza wananchi.

Nae Mkurugenzi wa Jiji hilo Bw.  Daudi Mayeji  alieleza kuwa kutokana na mradi wa mji mpya wa Pongwe kutotekelezwa vizuri, Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kushirikiana na vyuo vya Ardhi vya Tabora na Morogoro imeanza kutenga na kupima kwa ajili ya kuuza viwanja kwa wananchi.  
Alieleza kuwa viwanja hivyo vitauzwa na Halmashauri ya Jiji yenyewe  na vitakuwa na ukubwa unaozingati mahitaji halisi ya wananchi huku vikiuzwa kwa bei nafuu.

“Mradi huo mpya umezingatia miundombinu yote muhimu na jumla ya viwanja 4,700 tayari vimepimwa,” Alieleza Bw. Mayeji.
-MWISHO-

Captions
1. Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  (mwnye koti jekundu) akiangalia ramani ya viwanja vya makazi na biashara ya mradi wa mji mpya wa Pongwe katika ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Tanga. Upande wa kulia (mwenye miwani) ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Bw. Daudi Mayeji na aliyesimama (mwenye daftari) ni Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Bw. Joseph Mafuru, wengine ni wataalamu wa ukaguzi wa miradi walioambatana na Kaimu katibu Mtendaji.
2. Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Bw. Joseph Mafuru (mwnye koti jekundu) pamoja na maofisa kutoka tume ya mipango pamoja, Halmashauri ya Jiji la Tanga  pamoja na mfanyakazi wa Amboni Sisal Properties Limited (aliyesuka) wakiangali ukubwa wa eneo la Mradi wa Mji Mpya wa Pongwe (eneo halionekani pichani).
3. Sehemu ya eneo viwanja vya makazi na mbiashara katika Mradi wa Mji Mpya wa Pongwe.
4. Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  (mwenye koti jekundu) akioneshwa kitu kwenye ramani ya mradi wa mji mpya wa Pongwe na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya  Amboni Sisal Properties Limited (aliyesuka).
5.  Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Bw. Joseph Mafuru akiongea jambo kwa Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  wakati wa ziara ya Tume ya Mipango katika mradi wa mji mpya wa Pongwe jijini Tanga.
PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO