Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Gambia Atorokea Kusikojulikana


Mkuu wa tume huru ya uchaguzi nchini Gambia amekwenda mafichoni na jamaa yake akihofia maisha yake, kulingana na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC
Kwa mujibu wa ripoti ambazo hazikuthibitishwa, Alieu Momar Njai, ambaye alitangaza kushindwa kwa rais Yahya Jammeh kwenye uchaguzi wa urais wa mwezi jana, ametoroka kutoka nchini humo. Awali rais Jammeh alikubali kushindwa kwenye uchaguzi huo, lakini akabadili msimamo  baada ya muda mfupi na sasa amekataa kung’atuka mamlakani.
Kiongozi huyo wa Gambia sasa ameamuru vikosi vya usalama kuzingira afisi za tume ya uchaguzi. Hata hivyo mwana wa kiume wa Njai hakuweza kuthibitisha ikiwa baba yake ametoroka, lakini alimtakia heri popote alipo. Rais Jammeh, ambaye ameitawala Gambia kwa miaka 22, anatarajiwa kukabidhi mamlaka kwa Adama Barrow, ambaye ni mmliliki na mjenzi wa  majumba, ambaye alishinda kwenye uchaguzi wa urais uliofanywa  tarehe mosi mwezi wa Disemba kwa kujipatia aslimia 45 ya kura. Juhudi za kidiplomasia za kumshawishi  Jammeh kukubali kushindwa kwenye uchaguzi huo  hazijafanikiwa. Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya mataifa ya magharibi-ECOWAS ambayo ilianzisha harakati hizo , imetishia kutumia vikwazo kumshinikiza Jammeh kuondoka mamlakani.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO