Baadhi yawafanyakazi wa hoteli ya kitalii ya Parrot iliyopo
katikati ya Jiji la Arusha wameulalamikia uongozi wa hoteli hiyo
kuwatelekeza jijini hapa na kushindwa kuwalipa malimbikizo ya mishahara
yao ya zaidi ya sh,50 milioni tangu mwaka jana.
Mbali na malimbikizo hayo wafanyakazi hao wamedai fedha za malimbikizo
ya NSSF zaidi ya kiasi cha sh 15 milioni sanjari na kufukuzwa katika
hoteli ya Royal Court iliyopo Sakina Jijini hapa ambapo uongozi wa
hoteli hiyo uliwakodishia kama sehemu ya malazi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyakazi hao walisema ya kwamba
waliletwa jijini hapa mwezi Oktoba mwaka jana kutoka mikoa mbalimbali
nchini kwa lengo la kuja kufanya kazi lakini kinyume chake uongozi wa
hotelihiyo umeshindwa kuwalipa mishahara yao na sasa umewafukuza kazi
kinyemela.
David Sichinga ambaye ni meneja mapokezi alisema kwamba waliwasili
mwezi Oktoba mwaka jana na kukodishiwa sehemu ya malazi katika hoteli ya
Royal Court lakini cha ajabu uongozi wa hoteli hiyo umekuwa ukiwapiga
danadana kuwalipa mishahara yao tangu mwaka jana.
Ezra Ezekiel ambaye nimeneja utunzaji nyumba alisema kwamba yeye
ametokea mkoani Mwanza na hali ya maisha imekuwa ni ngumu jijini Arusha
kwa kuwa hajui anakula nini wala kulala wapi huku akisisitiza ameacha
familia mbali ambayo inamtegemea.
“Mimi nilichukuliwakutoka mkoani Mwanza nikaletwa kufanya kazi hapa
Arusha lakini cha ajabutumetelekezwa na sijui nitakula nini wala
kulala wapi kwani tumefukuzwahotelini na kazini tumeambiwa
tusikanyage”alisema Ezekiel
Naye, Benedict Machageambaye ni meneja wa chakula na vinywaji mkazi wa
jijini Dar es salaam alisema kwamba wanaiomba serikali
kuingilia kati madai yao kwa kuwa wanahisi ya kwamba uongozi wa hoteli
hiyo unalenga kuwapora haki zao.
Machage, alisema kwambakuna baadhi ya wafanyakazi wametoka kisiwani
Zanzibar na hawajalipwa hata sentitano tangu wawasili jijini Arusha
kufanya kazi huku akidai hali yao kimaishaimekuwa ngumu.
Mkurugenzi wa hotelihiyo, Abdallah Mshana alipoulizwa na gazeti
hili kuhusiana na madai hayo alisema kwamba anawatambua watu hao kama
waliwahi kufanyiwa usaili na sio kuajiriwa huku akiwataka waende
mahakamani endapo wana malalamiko.
“Mimi natambua kwambahao watu waliwahi kufanyiwa usaili na sio kwamba
waliajiriwa na kama wanamalalamiko waende mahakamani”alisema Mshana
Hatahivyo,mkurugenzi mtendajiwa kampuni ya Hospitality Concepts
International ambayo imepewa jukumu la kuajiri wafanyakazi hao na
kusimamia hoteli hiyo ,Macmillan Simba alikiri kuwatambua wafanyakazi
hao na sanjari na madai yao ya mishahara na michango ya NSSF na kusema kwamba kuna
matatizo ya kifedha yanayowakabili na pindi yakitatuliwa watalipwa
tufedha zao.
Simba,alisema kwamba waliwajulisha wafanyakazi hao kurejea makwao
mwishoni mwa mwaka jana kutokanana matatizo hayo ya kifedha lakini
baadhi yao waligoma na kuhusu kutimuliwa hotelini alikiri suala hilo na
kudai kwamba wameshatangaza mgogoro na mwajiri wao na hivyo ni vigumu
mwajiri huyo kuendelea kuwalipia hoteli.
CHANZO: WOINDE SHIZA
0 maoni:
Post a Comment