Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NHIF Tanga yalipa Bilioni 5 kwenye vituo vya Afya mwaka 2015/2016


“NHIF Tanga yalipa Bilioni 5 kwenye vituo vya Afya mwaka 2015/2016

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umefanikiwa kulipa vituoni madai yanayotokana na huduma za afya kwa wakati  zaidi ya bilioni 5.1 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 sawa na asilimia 148.

Malipo hayo yamesaidia huduma kuboreshwa kwenye vituo mbalimbali ikiwemo watoa huduma kuhamasika na uelewa juu ya mfuko huo .

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Ally Mwakababu (Pichani )wakati akitoa taarifa ya utendaji wa mfuko huo kwa waandishi wa habari mkoani hapa.

Ambapo alisema kwenye kipindi cha mwaka 2014/2015 walilipa kiasi cha zaidi ya bilioni 3.5 hali inaonyesha ongezeko kwa mwaka huu.

Alisema pamoja na malipo kuongezeka lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma za afya vijijini imekuwa kikwazo sanjari na upatikanaji wa dawa vituoni.

Aidha alisema lakini pia kuongezeka kwa magonjwa yakiwemo ya ukimwi ikiwemo upungufu wa watumishi katika sekta ya afya.

 “Lakini changamoto nyengine ni ugonjwa wa ukimwi kwa wanachama ni chanzo cha magonjwa nyemelezi na lakini pia halmashauri hazijachangamkia mikopo ,vifaa tiba,ukarabati na dawa kwenye vituo vyao “Alisema.

Aidha alisema katika kuhakikisha uhai wa mfuko huo unakuwa endelevu mfuko huo uliamua kufanya ukaguzi kwenye vituo vinavyoashiria wizi na udanyanifu.

“Katika kipindi hicho mfuko umefanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya milioni 83.6 kutokana na ukaguzi maalumu 29 zilifanyika kwenye vituo 22 kutokana na kuona vinaashiria vya hujuma au uadanyanyifu wa huduma kwa wanachama wa Bima ya Afya “Alisema.

 “Kaguzi hizo zilifanyika kwenye vituo vya serikali 10 sawa asilimia 45,vituo vya madhehebu ya dini 8 sawa na asilimia 36 na vituo vya watu binafsi 4 sawa na asilimia 19 “Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tangaraha
Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO