Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

LEMA ARUDISHWA TENA MAHABUSU BAADA YA JAMHURI KUIPELEKA KESI YAKE MAHAKAMA YA RUFAA

Mbunge wa Arusha Mjini akipungia kwa kuwapungia mkono  wananchi waliojiokeza  katika viwanja vya Mahakamu Kuu Arusha jana kusikiliza shauri lake akielekea kwenye gari kurudishwa gerezani Kisongo jana. Picha na Moses Joseph

Mmoja wa mwakili wanaomtetea Lema,WakiliJohn Mallya akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wenzake jana kuelezea kilichotokea mahakamani ambapo ameeleza kwamba kilichofanyana wanasheria wa Jamhurini kukata rufaa juu ya rufaa jambo ambalo sio sahihi kisheria na kupelekea Lemakuendelea kusota rumande bila sababu za msingi kisheria. Picha na Vero Ignatus


Mke wa Mbunge wa Arusha Mjini ambaye mume wake Godbless Lema anakabiliwa na kesi ya uchochezi Neema Tarimo Lema akizungumza jambo na dereva wa Mbunge huyo Haleluya Natai nje yaviwanja vya Mahakama Kuu Arusha jana 

Mh Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjinia amelazimika kurudishwa tena rumande baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kushindwa kutoa uamuzi kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani kupinga mbunge huyo kupewa dhamana.

Jaji wa Mahakama kuu ya Arusha aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Salma Magimbi ameshindwa  kutoa maamuzi kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa ya mahakama kuu ya Rufaa kupinga dhamana dhidi ya  Lema na kueleza kuwa hana mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kutokana na uamuzi huo na hivyo kusababisha mbunge Lema kurudishwa tena rumande.

Kwa upande wa Wakili mtetezi wa Mbunge Lema John Mallya akielezea mwenendo wa kesi hiyo kwa niaba ya mawakili wenzake amesema wamesikitishwa na uamuzi u
liotolewa mahakamani leo kwani Jamhuri wangepaswa kutoa uamuzi wa dhamana na siyo kukata rufaa juu ya rufaa.

Amesema jambo hilo linalobishaniwa na upande wa Jamhuri lipo wazi na kwamba wanajipanga kwenda katika mahakama kuu ya rufaa kabla yao ili shauri hilo liweze kusikilizwa na mteja wao amekubaliana nao.

Mbunge huyo amerudishwa tena Rumande hadi hapo kesi hiyo itakaposikilizwa tena ambapo mpaka sasa amefikisha siku 61 akiwa mahabusu.


STORI: VERO IGNATUS
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO