Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

YANGA YATOLEWA NA SIMBA MAPINDUZI CUP 2017 KWA MIKWAJU 4-2 BAADA YA KUTOSHANA NGUVU MUDA WA KAWAIDA
CHANZO: By Gift Macha, Mwananchi
Zanzibar. 
Penalti nne zimetosha kuifanya Timu ya Simba kuingia fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuicharaza Yanga iliyoambulia mbili.
Simba sasa itacheza na Azam baada ya kuizima Yanga kwa mikwaju ya penalti katika mchezo mkali wa nusu fainali ya pili uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Baada ya Simba kupata penalti tatu zilizofungwa na Jonas Mkude, kipa Daniel Agyey na Muzamir Yassin huku Yanga zikifungwa na Simon Msuva na Thaban Kamusoko ilibakia moja kila upande.
Ikawa sasa kila mmoja anamwangalia Janvier Bokungu, ambaye alikuwa anakwenda kupiga penalti ya tano kwa Simba hapo tayari Method Mwanjali (Simba) na Deo Munish na Haji Mwinyi walikuwa wameshakosa penalti zao.
Awali kabla ya mikwaju hiyo kila upande ulifanya mashambulizi ya kushtukiza na kutegeana, Simba ilicheza kwa kujihami zaidi ikitumia mfumo wa 4:5:1 huku Yanga ikitumia 3:5:2.
Yanga ilifanya badiliko moja pekee katika kikosi chake kilichopoteza mchezo uliopita dhidi ya Azam FC wakati Simba ilikuwa na mabadiliko ya wachezaji watatu katika kikosi kilichocheza mechi ya mwisho na Jang’ombe Boys.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO