Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MALISA: UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA UPOTOSHAJI KUWA MHE.LIJUALIKALI AMELILIA SALUTI.

Imeandikwa Na Malisa J. Godlistern
Kuna taarifa potofu inaenezwa hasa na vijana wa CCM kuhusu kauli ya Mhe.Peter Lijualikali kwa Waziri wa mambo ya ndani Mhe.Mwigulu Nchemba alipofanya ziara wilayani Kilombero. Taarifa hiyo imeambatanishwa na kipande cha video ya Mhe.Lijualikali inadai kuwa Mbunge huyo amelilia kupigiwa saluti na askari polisi.
Kwanza niseme kuwa unahitaji PhD ya ujinga ili uweze kuamini kwamba Mbunge anaweza kulilia saluti ambayo ni haki yake kisheria. Suala la Mbunge kupigiwa saluti sio zawadi, ni takwa la kisheria na kikatiba. Na hata Mhe.Mwigulu alipojibu hoja hiyo alimuita OCD wa Kilonbero na kumuagiza kwamba ni wajibu wa Polisi wote kuanzia OCD na walioko chini yake kumsalimia Mbunge kwa saluti, awe mbunge wa CCM au wa vyama vya upinzani.

Na Mwigulu akaongeza kuwa hakuna mbunge nusu na mbunge kamili. Kuwa Mbunge wa Upinzani haikufanyi kuwa mbunge nusu na kuwa mbunge wa CCM haikufanyi kuwa mbunge kamili. Wote ni wabunge na wanastahili haki na heshima sawa. Hivyo ndivyo waziri Mwigulu alivyowaeleza polisi.

Kwahiyo Mhe.Lijualikali hakulilia saluti bali alikua akiongelea dharau ya Polisi kwa wananchi na viongozi hasa wa upinzani na akatumia issue ya saluti kama mfano mmoja wapo wa kuelezea dharau hizo. Zipo dharau nyingi zinazofanywa na polisi kwa wananchi na viongozi wao.

Kwa mfano Polisi waliwahi kuvamia kikao cha baraza la madiwani wilaya ya Kilombero na kumtoa Mhe.Lijualikali nje kwa nguvu. Hizi ni dharau kwa sababu polisi si wajumbe wa baraza la madiwani, na hawaruhusiwi kuingia ndani bila baraza kutengua kanuni na kuwaruhusu kuingia. Lakini hawakufuata taratibu bali waliingia kibabe na kumtoa. 

Tumeshuhudia pia bungeni polisi wakiingia na kuwatoa wabunge wa upinzani kwa nguvu bila kanuni kutenguliwa.
Kwahiyo Lijualikali alijenga hoja kwamba ikiwa Polisi wanashindwa kuheshimu viongozi je wataweza kuheshimu wananchi? Ikiwa wanaweza kufanya vitendo vya kibabe kwa viongozi, je wananchi itakuaje? Kama polisi wanadharau, wanapuuza na kuwafanyia ubabe viongozi je vipi kuhusu wananchi wa kawaida? Hiyo ndio ilikua hoja ya Lijualikali na sio kulilia saluti kama inavyoenezwa na vijana wa propaganda wa CCM.

Tena Lijualikali alihoji juu ya misaada mbalimbali inayotolewa na wabunge kwa kushirikiana na wananchi kwa jeshi la polisi. Kwa mfano ujenzi wa vituo vya polisi. Wabunge wengi wamejitolea fedha zao za mfuko wa jimbo kujenga vituo vya polisi. Pesa hizo wangeweza kuzipeleka kwenye miradi mingine.

Lijualikali nae ametenga fedha kwenye mfuko wa jimbo kusaidia ujenzi wa vituo vya polisi kwa kushirikiana na wananchi (kuwahamasisha wachangie). Lakini kama Polisi wanapiga viongozi, hawawaheshimu, wanadharau raia na kuwanyanyasa, je inawezekana wananchi kutoa pesa zao mfukoni kuchangia ujenzi wa vituo vya polisi? Unawezaje kumchangia mtu anayekupiga, anayekudharau, anayekunyanyasa? Hiyo ndio ilikua hoja ya Lijualikali.

Kwahiyo kama Polisi wanataka ushirikiano kutoka kwa wananchi na viongozi hasa wa upinzani ni lazima wajenge misingi ya kuheshimiana. Polisi anapaswa kumheshimu kila raia na kuwaheshimu viongozi wa upinzani sawasawa na wanavyowaheshimu viongozi wa CCM.

Polisi wanatakwa na sheria kuwapigia saluti wabunge wote lakini wamekua wakiwapigia saluti wa CCM na kuwaacha wa vyama vya upinzani, hii si sawa hata kidogo. 

Tunajenga double standards katika jamii moja, kitu ambacho ni kibaya sana. Polisi waheshimu viongozi wote, na wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa. Wakifanya hivyo nao wataheshimiwa na kupewa ushirikiano na misaada na jamii katika mambo mbalimbali. Hiyo ndio ilikua hoja ya Lijualikali na si kulilia saluti.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO