Madaktari wamekataa kiwango cha nyongeza ya mshahara walichoahidiwa na rais Uhuru Kenyatta ili kusitisha mgomo unaoendelea na badala yake kushinikiza utekelezaji kikamilifu wa makubaliano ya nyongeza ya mshahara ya mwaka-2013. Wakihutubia wanahabari jijini Nairobi hivi leo, maafisa wa baraza la ushauri la chama cha wahudumu wa afya na wataalam wa meno walisema hawatakubali chochote ila kutekelezwa kwa makubaliano hayo ya mwaka 2013. Maafisa hao walisema makubaliano hayo yamejikita kwenye misingi ya sheria na serikali inafaa kuyatekeleza.
Wakati huo huo maafisa hao wanatarajiwa kuandaa mkutano na wizara ya fedha leo alasiri kujadili jinsi makubaliano hayo ya pamoja yatakavyotekelezwa. Nyongeza hiyo ambayo serikali imesema itagharimu walipa ushuru shilingi bilioni-4 kila mwaka ilipendekezwa mjini Mombasa siku ya Jumatano.
CHANZO: KBC TAIFA
0 maoni:
Post a Comment