Na.Vero Ignatus Arusha.
|
Waongoza utalili wanaosaidia watalii kupanda milima wameiomba serikali kutazama upya malipo wanayopewa katika utekelezaji wa kazi zao kwasababu hayalingani na ugumu wa kazi wanazofanya kuhudumia watalii.
Kwa sasa waongoza watalii hao wanalipwa wastani wa kiwango cha dola 10 za kimarekani kwa siku ,kiasi ambacho hakilingani na kazi wanazozifanya.
Hayo yamesemwa na katibu wa waongoza watalii Immanuel Mollel katika sa kongamano la mambo ya utalii na uhifadhi kwa waandishi wa habari na wadau wa utalii inayofanyika kwa siku mbili katika hotel ya Palace iliyopo Jijini Arusha.
Katibu huyo amezitaja changamoto mbalimbali ambazo wanazipitia ni pamoja na kukosa mikataba ya ajira, wao kulazimika kununua leseni ili waweze kuwaongoza watalii, uharibifu wa mazingira na tabia nchi pamoja na ujangili.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha wabeba mizigo ya watalii Loshiye Mollel amesema changamoto kubwa wanazozipata ni pamoja na mazingira magumu wanayokabiliana nayo katika utendaji kazi wao.
“wakati tunapokuwa mlimani umebeba mzigo wa mgeni kuna magonjwa ya mlimani ,sasa namna ya kumuokoa huyu mbeba mizigo ya mtalii ni shida sana ,kwani itawalazimu wale ambao wapo kule juu mlimani wakushushe kwa machela hadi chini ,huko napo unakutana na changamoto nyingine hakuna gari kwani magari yapo mawili tu"
"Tupo wabeba mizigo zaidi ya 28,000,kwa siku moja tunakuwa mlimani zaidi ya wabeba mizigo (porters) 4000 au 3000,tunaiomba serikali kutuongezea magari ili kuwepo urahisi wakati wa kumsaidia mbeba mizigo ya watalii anapopata shida akiwa mlimani) mlimani,a
0 maoni:
Post a Comment