Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan akitoa ufafanuzi kuhusu uwekaji wa kituturi cha kupigia kura wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Januari 22, 2017 leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan akionyesha mfano wa namna ya kuweka vituturi vya kupigia kura vituoni ili kuwawezesha wananchi kupiga kura kwa wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Januari 22, 2017.
Kaimu Naibu –Uendeshaji wa Uchaguzi, Bi. Irene Kadushi Tutah akiwasilisha mada kuhusu Kujumlisha na Kutangaza Matokeo ya Ubunge na Madiwani wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo utakaofanyika Januari 22, 2017.
Washiriki wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kutoka Kanda ya Kaskazini na Pwani wakiendelea na mafunzo ya kuwajengea uwezo wasimamizi hao wakati uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Januari 22, 2017.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo Januari 22, 2017 mjini Dodoma. Picha na Aron Msigwa - NEC
0 maoni:
Post a Comment