Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RC Gambo akabidhi mfano wa hundi ya sh mil 425 ya mikopo kwa kina mama kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akikabidhi mfano wa hundi  ya shilingi milion 425 kwa mwakilishi wa vikundi vya akina mama Jijini Arusha katika  ufunguzi wa semina maalumu kwa kina mama wajasiriamali, fedha ammbazo zimetolewa na Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Semina hiyo imefunguliwa na Mkuu wa Mkoa na itafungwa na Meya Wa Jiji la Arusha Mstahiki Kalisti Lazaro leo saa 10 jioni.

Fedha hizo mil 425 hii ni awamu ya pili ya mikopo kwa wajasiliamali wa Jijini Arusha kukabidhiwa pesa  kutoka kwenye fedha za makusanyo ya Halmashauri ya Jiji. 

Blogu hii inapongeza jitihada za Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya, bila kusahau Halmashauri ya Jiji la Arusha inayoongozwa na CHADEMA kuweza kufanikisha utoaji mikopo kama kanuni zinavyoagiza, jambo ambalo limekuwa gumu kutekelezeka maeneo mengi nchini.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO