Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MEYA WA JIJI LA ARUSHA KALISTI LAZARO ALIVYOZINDUA KAMPENI ZA MGOMBEA WA CHADEMA NGARENANYUKI JANUARI 9, 2017


Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro ambaye pia ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, akizungumza siku ya Januari 9, 2017 katika mkutano wa Uzinduzi wa kampeni za mgombea wa CHADEMA Aminiel Furahini Mungure (mwenye skafu) kuwania Udiwani Uchaguzi Mdogo Kata ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru na kuwataka wananchi kuwapuuza wateule wa Rais ambao wamekuwa wakiacha majukumu yao na kuwasumbua madiwani wa chama chake
 Meya Kalisti ameonya matumizi mabaya ya Rasilimali za umma yakiwemo Magari Ya Serikali na idara zake  kwa shughuli za siasa ya chama kimoja.

Mgombea wa CHADEMA kuwania udiwani katika uchaguzi mdogo Kata ya Ngarenanyuki Mh Aminiel Furahini Mungure akijinadi kwa wananchi hawaonekani pichani siku ya Januari 9, 2017


Sehemu ya wananchi waliojitokeza mkutanoni hapo

Katibu wa CHDEMA Mkoa wa Arusha Mbaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Siha (CHADEMA) Dr Godwin Mollel (katikati) wakakti wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za kuwaniaudiwani katika uchaguzi mdogo Kata ya Ngarenaanyuki wilayani Arumeru siku ya Januari 9, 2017

Mgombea wa CHADEMA udiwani Kata ya Ngarenayuki katika uchaguzi mdogo wa kata hiyo Aminiel Furahini Mungure akiwasili eneo la mkutano na kupungia wananchi waliokwisha kuwasili siku ya Januri 9, 2016. Mwingine anyesalimia ni Mbunge wa Siha Dr Mollel

Mgombea wa CHADEMA katika uchaguzimdogo kuwania udiwani Kata ya Ngarenanyuki, Aminiel Furahini Mungure akiwa na wananchi wanaomuunga mkono katika uzinduziwa Kampeni yake Januari9, 2017

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Katibu wa chama hicho Kanda ya Kaskazini, Mh Amani Golugwa akihutubia mkutanoni hapoMsafara wa pikipiki kuhamasisha shamrashamra za uzinduzi wa kamapeni za mgombea wa CHADEMA kuwani udiwani katika uchaguzi mdogounaotarajiwa kufanyika baaddae Kata ya Ngarenayuki wilayani Arumeru.ANGALIA VIDEO YA MEYA KALISTI AKIHUTUBIA MKUTANONI HAPO
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO