Na Woinde
Shizza,Arusha
WAFANYABIASHARA wa maduka jijini Arusha,wameilalamikia halmashauri
hiyo ,wakipinga notisi ya miezi mitatu waliopewa ,inayowataka kuondoka
katika maduka hayo,ifikapo Machi 30,mwaka huu, kufuatia maduka yao
kudaiwa kumilikiwa ma madalali na hivyo kuikosesha mapato
halmashauri
hiyo .
Aidha walidai kuwa hawapo tayari kuhama na hawatambuni notisi hiyo na
wataendelea kufanyabiashara zao kama kawaida kwa kuwa wamekuwa
wakilipa mapato ya halmashauri kama inavyopaswa.
Wakizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari,uliolenga kujadili
notisi hiyo, mwenyekiti wa wafanyabiashara hao jijini Arusha,Loken
Masawe alisema halmashauri hiyo imetoa notisi kwa lengo la kutangaza
tenda kwenye maduka hayo ,hatua hiyo walisema haiwatendei haki kwani
wengi wao walijenga maduka hayo na hatua hiyo itawasababisha
washindwe kulipa fedha walizokopa kwenye mabenki mablimbali.
‘’Sisi hatujakataa tenda wanayotaka kutangaza kwenye maduka hayo ila
kwanini wanataka kuweka watu wao ili sisi tufe njaa ,familia zetu
tutazilisha nini ,tunachosema tenda hii sio halali na
hatutakubali’’alisema Masawe
Wafanyabiashara hao ambao ni zaidi ya 1200 wanaomiliki maduka katika
maeneo mbalimbali katika jiji hilo,walienda mbali zaidi kwa kumtaka
rais John Magufuli kuingilia kati ili kuwanusuru na kadhia hiyo
inayolenga kuwadhalilisha wao na familia zao
Naye mfanyabiashara Meja willson Lukumamu alisema kuwa walijenga
maduka katika eneo la stand ndogo kwa gharama zao ,wakati huo eneo
hilo lilikuwa pori na kwamba hadi sasa hawakuwahi kurejeshewe gharama
zao .
‘’Huu mpango unaofanywa na manispaa ni batili kwani sisi kama
wafanyabiashara hatujawahi kushirikishwa ,tunachotaka usitishwe na
biashara zetu ziendelee kama kwaida’’alisema
Akizungumzia malalamiko ya wafanyabiashara hao,Meya wa jiji la
Arusha,Kalisti Lazaro alisema kimsingi madai yao hayana msingi, kwani
mpango huo ni utekelezaji wa maoni ya tume iliyoundwa na mkuu wa mkoa
wa Arusha,Mrisho Gambo iliyolenga kuchunguza uhalali wa umiliki wa
maduka hayo.
Kalisti alisema kuwa halmashauri hiyo haitarudi nyuma katika mpango
huo kwani imekuwa ikipozeza zaidi ya shilingi bilioni 2.1 kutokana na
maduka hayo kumilikiwa na madalali ambao huwapangishia wafanyabiashara
kwa gharama kubwa huku halmashauri hiyo ikipata mapato kiduchu.
‘’Baada ya tume kuundwa na mkuu wa mkoa ,Mrisho Gambo
ilifanyakazi ya
kuchunguza uhalali wa umiliki wa maduka hayo na kubaini kuwa wamiliki
wa maduka hayo wengi wao ni madalali na wamekuwa wakipangisha maduka
hao kwa gharama kubwa na kuilipa halimashauri kiwango kidogo’’alisema
Meya
Alitolea mfano mfanyabiashara Morice Makoi kuwa anamiliki maduka 27
,eneo la kituo cha daladala na amepangisha kwa shilingi laki tano hadi
laki nane kwa duka moja huku yeye akiilipa halmashauri hiyo shllingi
50,000 kwa mwezi,jambo ambalo alisema halikubaliki.
Alisisitiza kuwa halmashauri hiyo haina mpango wa kuwafukuza
wafanyabiashara hao ila inachofanya ni kutangaza tenda upya ili kila
mmoja aweze kuomba umiliki na atakayeshinda atakabidhiwa duka lake kwa
mkataba maalumu .
Aliwataka wafanyabiashara hao kuacha kulalamika badala yake wafuate
taratibu ikiwemo kuleta maombi mapya ya barua yatakayoambatana na TIN
namba,Lesen,na kwamba watakao kidhi vigezo hivyo watakabidhiwa duka
mara moja.
0 maoni:
Post a Comment