Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Moto Wateketeza Maduka Ya Biashara Arusha

Moto mkubwa umeteketeza nyumba ya biashara yenye maduka matano eneo la Mianzini Jijini Arusha.

Moto huo ambao chanzo chake hakijaweza kurhibitishwa na Jeshi  la Polisi bado, ingawa mashuhuda wanadai ni shoti ya umeme na unadaiwa kuanza majira ya saa  12 alfajiri na kuunguza sehemu kubwa nyumba ya biashara inayomilikiwa na Emanuel Hagai na Benjamin Hagai yakiwemo maduka matano ya biashara mojawapo likiwa ni duka kubwa la Mianzini Mini Supermarket linalomilikiwa na Elia Wilbard Oiso.

Wamiliki wa maduka mengine tisa kwenye nyumba hiyo walifanikiwa kuokoa baadhi ya mali.
Akizungumza na Blogu hii eneo la tukio, Diwani wa Kata ya Levolosi ambapo uharibifu huo umetokea ametoa pole sana kwa wote waliopatwa na janga hilo na kuwaombea kwa Mwenyenzi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi hiki wakati jitihada nyingine zikiendelea kufanyika.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO