Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Awamu ya Pili Mikopo: Jiji la Arusha latoa Sh mil 624 Mikopo kwa Vijana na Kina Mama

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akizungumza wakati wa mafunzo na makabidhiano ya hundi za mfano kwa vikundi vya kina mama na vijana Jijini Arusha leo ambaye amesema tangu aanze kuongoza Halmashauri hiyo jumla ya Sh 1.2 billion zimekweishatolewa kwa njia ya mikopo kwa vikundi mbalimbali na kuongeza kuwa Halmashauri yake itaendelea kutoa mikopo zaidi kwa wananchi wote wa Jiji la Arusha na kutoa rai kwa wananchi wote kuunda vikundi ili waweze kufaidika na mikopo hii.
Arusha
Halmashauri ya Jiji la Arusha inayoongozwa na CHADEMA hii leo imetoa jumla ya TShs 624,000,000,00 za mikopo kwa vijana nakina mama ndani ya Jijila Arusha. Kati ya hizo Sh 425mil ni kwa ajili ya wanawake na Sh 199,mil ni kwa ajili ya Vijana kutoka katika fungu la mapato yake ya ndani.

Utoaji huu wa mikopo ni awamu ya pili kwa Halmashauri kutoa mikopo kwa ajili ya vikundi mbalimbali vya kijasiriamali. Mara ya kwanza jumla ya Sh 405mil zilitolewa kwa kina mama na hivyo kufanya jumla ya Sh 1.24bil zimetolewa kama mikopo kusaidia jamii ikijwamue kicuhumi tangu Halmashauri hii iwe chini ya CHADEMA.

Mbali na kupewa mikopo hiyo, wanufaika hao wamepatiwa semina maalumu kuwawezesha kuwa na matumizi bora ya fedha hizo.

Mstahiki Meya amefunga mafunzo hayo ambayo yalifunguliwana Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo mapema asubuhi kwa kukabidhi hundi ya mfano ya Sh 425mil kwa kina mama.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO