Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TAMASHA LA ARUSHA TOURISM FESTIVAL LAFANA ARUSHA, WATOTO WADOGO NAO WASHIRIKI NA MBIO


Mgeni rasmi katika tamasha hilo Afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno akimkabidhi mmoja kati ya washindi wa kwa upande wa wanawake mbio za kilometa 3000 zawadi,ambapo mshindi wa kwanza Anjeline Tsere alitumia dakika 9:39.96,Jacline Sakilo alitumia dakika 9:44.13,na wa tatu Secilia Ginoka ametumia dakika 9:45 .Picha na Vero Ignatus Blog

Pichani ni Katibu wa chama cha riadha mkoa wa Arusha Alfred Shahanga,ambaye pia ni muaandaaji wa Arusha Tourism Festival Picha na Vero Ignatus Blog. 
Pichani Mussa Juma ambaye ni  Mkurugenzi wa Arusha Media  ambaye ni muandaaji wa Arusha Tourism Marathon Festival.
Wa kwanza kushoto ni mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha,Andrew Ngobole ambaye pia ni mmoja wa waandaaji wa mashindano hayo kutoka Arusha media akisalimiana na katibu wa chama cha riadha mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.
Kikundi cha Ngoma kutoka jijini Arusha kijulikanancho kama Mtikisiko sanaa group wakitoa burudani katika mashindano hayo ya Arusha Tourism Marathon.Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya wadau na washiriki katika mashindano katika tamasha la Arusha Tourism Marathon wakiwa wanafuatailia yanayoendelea uwanjani hapo.Picha na Vero Ignatus Blog

Mshindi wa Arusha Tourism Marathon Festival  akiwa anamalizia mbio za kilomita 5000 Emmanuel Giniki ambate amepewa zawadi ya shilingi 200,000 pamoja na kupatiwa bonansi ya kuongoza njia shilingi 50,000. Picha na Vero Ignatus Blog.

Mshindi wa pili wa mbio za kilometa 5000 za Atusha Tourism Marathon  Gabriel Geay ametumia dakika 14:05:08.Picha na Vero Ignatus Blog
Wakwanza kutoka kulia ni mkurugenzi wa Arusha Media Musa Juma akimnyanyua mkono mshindi wa Arusha Tourism Marathon Emmanuel Giniki katikakatika mashindano hayo,Kutoka kulia ni Katibu wa chama cha Riadha mkoani Arusha Alfredy Shahanga ,akifuatiwa na mshindi wa tatu Ismail Juma ambaye alimaliza mbio hizo kwa kutumia dakika 14:11.60,akifuatiwa na mshindi wa pili Gabriel Geay  .Picha na Vero Ignatus Blog


Afisa michezo Jiji la Arusha Benson Maneno wakwanza kushoto akijiandaa kuzindua mbio maalum za watoto wadogo walioshiriki katika Arusha Tourism Marathon akiwa pamoja na mwenyekiti wa Marathon mkoa wa Arusha 
Watoto wakiandwaliwa tayari kwa kukimbia mbio za mita hamsini leo katika uwanja wa Shekh Amri Abeid,na wao wameshiriki katika Arusha Tourism Marathon.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wakwanza kulia namba 043ndiye mshindi wa kwanza kwa wanawake katika mbio za kilometa 200 ambapo ametumia dakika 29:04,akifuatiwa na mshindi wa pili aliyepo katikati Susan Patric kutoka Arusha miaka( 20)ambaye ametumia dakika 29:31 na mshindi wa tatu ni Neema Kasunda (20)ametumia dakika 29:89.Picha na Vero Ignatus Blog
Mtoto huyu naye ameshiriki mbio mita 50 katika tamasha la Arusha Tourism Marathon .Picha na Vero Ignatus blog


Haji Mbuguni kutoka kutoka Chama cha waongoza Utalii Tanzania ,ambaye anashughulika naIdara ya mazingira, uhusiano,na uhamasishaji ,yeye nae ni mdau wa utalii na ameshiriki katika tamasha la Arusha Tourism Marathon Festival (Utalii na michezo inawezekana)Picha na Vero Ignatus Blog.Na.Vero Ignatus ,Arusha


Tamasha la Arusha tourism marathon limefanyika Leo jijini Arusha ikiwa ni awamu ya pili kufanyika mkoani haha ambapo mashindano hayo yameandaliwa na Arusha Media, Shahanga sport promotion Chini ya udhamini wa Tanapa.

Tamasha hilo limewashirikisha wanariadha kutoka mkoa wa Arusha, Manyara,pamoja na Kilimanjaro ambapo tamasha hilo likiwa limebeba kauli mbiu ya piga vita ujangili, tembelea Hifadhi zetu.


Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Afisa michezo wajiji la Arusha Benson Maneno ambapo amesema kuwa riadha imeutoa mkoa wa Arusha kimasomaso na Tanzania kwa ujumla michezo mingine bado imedorora

Amekipongeza chama cha riadha mkoa wa Arusha na kuwataka kuongeza juhudi zaidi kwani michezo ni ajira,hujenga mwili kiafaya ,pia michezo humtambulisha mtu kitaifa na kimataifa pia, amewataka vijana kuchangamkia fursa hayo.

Katibu wa riadha mkoa wa Arusha kuwa Alfred Shahanga ambapo pia ni muandaaji mwenza wa Arusha Tourism Festival amesema kuwa mashindano hayo yalianza mwaka 2015 walianza na mbio za barabarani huku safari hii wameamua kurudi uwanjani ili kuhamasisha mbio fupifupi ambazo kuwamuda mrefu zimesahaulika.

"Mashindano haya kwetu sisi yameonyesha ufanisi mkubwa kwani mshindi wa kwanza katika mbio za mita 5000 ameweka rekodi ya uwanja namaanisha muda aliokimbia ni rekodi ya uwanja huu."alisema Shahanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Arusha Media Mussa Juma amesema kuwa lengo kubwa la mashindano hayo ni kuhamasisha michezo katika mkoa wa Arusha pamoja na kuutangaza Utalii wa ndani

"Tumewashirikisha watoto wadogo katika mashindano haya kwani hawa nimabalozi wabaadae ambao watakuja kupiga vita ujangili,watawahamasisha kizazi kijacho michezo , na watautangaza vyema utalii wandani hapo badge."alisema Mussa.


Mashindano hayo yameambatana na utoaji wa zawadi kwawashindi ambapo wasindi wa mbio za kilometa 3000 kwaupande wanawake mshindi wa kwanza alipewa zawadi ya shilingi 150,000 na wale wa mbio za kilomita 5000 mshindi wakwanza amepatiwa zawadi ya shilingi 200,000.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO