Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MOUNT MERU RICKERNEST MUSIC BANDI YAJA KWA KASI YAAIDI KUFANYA MAPINDUZI YA MUZIKI WA DANCE HAPA NCHINI


 Rais wa bendi ya  Mounti Meru Rickernest Music Band Fabrice Kinyenya (kulialia) Akiwa anaimba katika usiku wa kuwatambulisha bendi hiyo wakazi wa jiji la Arusha
 Wanamusiki wa bendi ya Mounti Meru Rickernest Music Band wakiwa wanaonyesha kiwango chao ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha




 waimbaji wa bendi ya  Mounti Meru Rickernest Music Band wakiwa fanya yao

 Wanenguaji wa bendi ya Mount meru Rickernest Music Band wakifanya yao

 Rais wa bendi akifanya mambo ndani ya ukumbi wa Triple A
 wakwanza kulia ni mmoja wa wakurugenzi wa bendi ya  Mount meru Rickernest Music Band Akifatilia onyesho ,wa pili kushoto ni mkurugenzi mwingine wa bendi hiyo Prisca Aloyce wote wakiwa wanafatilia kwa makini onyesho

Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

Bendi mpya  ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mount Meru Ricknest music bandi  imezinduliwa rasmi mkoani Arusha  huku ikiwaaidi  huku ikiwaaidi wapenda mziki wa dance burudani isiokuwa na mpinzani

Akiongea na waandishi wa habari jana  mmoja wa wakurugenzi wa bendi hiyo Ernest mlolere  alisema kuwa kwa sasa wameitambulisha bendi hiyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha tu na wanataajia   kuzindua bendi hiyo rasmi katika siku yawapendanao (valentine day ) hapa hapa jijini Arusha

Alibainisha kuwa bendi hiyo ipo chini ya wakurugenzi watatu akiwemo  yeye mwenyewe Erinest Mlolere ,Denis  Kaiza  pamoja na  Prisca Aloyce ambapo wamekaa chini na  wakaamua kuanzisha bendi hiyoili kuweza kuwapa burudani wakazi wa mkoa wa Arusha ,ambao wamekuwa wakikosa  burudani  ya bendi ya uhakika kwa kipindi cha mda mrefu



Alisema kuwa kumekuwa na bendi jijini hapa lakini  zimekuwa hazikoshi nyoyo za wapenzi wao wa musiki wa dance hivyo wameona wawaletee wanamusiki wenye uzoefu ,wenye vipaji vya kutosha ili wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na jirani  kuweza kupata burudani



Aidha aliongeza kuwa  bendi hii atakaa Arusha tu bali itakuwa inatembea mikoa mbalimbali ili kuweza kuwapa burudani wapenzi wa music wa dance wan chi nzima .



“tumejipanga vyema   tunaweza na tunauhakika ujio huu wa bendi hii utawafurahisha na kuwashika wapenzi wengi wa music wa dance ,kwani wanamusic ambao wapo katika bendi hii ni wazuri na wanavipaji vya kutosha nathani unajua kabisa ukiwa na kitu kizuri lazima watu wakipendi naamini kabisa wanamziki wetu wapenzi wa bendi watawapenda .



Alibainisha kuwa katika bendi hii pia kuna wana music kutoka katika bendi maarufu za nje ambapo alitaja baadhi ya wanamusic  waliotoka katika bendi za nje kuwa ni pamoja na rais wa bendi Fabrice Kinyenya (kulialia) ambapo yeye ametoka katika bendi ya  Ferre Gola  pamoja na Katoto (Tanesco) ambaye yeye ametoka katika bendi ya  Fally Ipupa wote .



Aliongeza kuwa wanajua kabisa kuna bendi zilizotangulia  hapa nchini na zinaaminika ila kwa jinsi walivyojipanga yeye na wanamusic wake anaimani kabisa watazipita bendi zote zilizopo hapa nchini na hata zile zilianzishwa hivi karibuni zilizopo jijini hapa.



 “sasa ivi tupo katika harakati za kupanga siku ya uzinduzi rasmi  wa bendi hii ila hii leo tumekuja kuwaonyesha wakazi wa mkoa wa Arusha kuwa kunabendi inayopiga vizuri sana iliopo hapa  mkoani kwao ,na kwakuwa ni nyumbani tumejipanga kila siku ya jumamosi kuwapa burudani ambapo tutakuwa tunapiga katika ukumbi wa triple A  Alisema  Mlolere



Kwa upande wake Rais wa bendi hiyo Fabrice Kinyenya (kulialia) alipoongea na waandishi wa habari  alisema kuwa wamejipanga vilivyo kuwapa wapenzi wa musiki wa dance burudani  ya uhakika ambayo itamkosha kila mtu nyoyo.



“mimi sipendi kuongea sana napenda kufanya vitendo zaidi ,wasanii wangu wapo vizuri nanachosema tu ni wapenzi wa musiki wa dance wasubiri kupata burudani ya nguvu yenye viwango vya kimataifa ,hapa ni kazi tu hakuna maneno mengi “alisema Fabrice



Alisema kuwa hadi sasa wameshatunga nyimbo za bendi na watazitambulisha siku ambayo bendi inatambulishwa rasmi ,huku akibainisha kuwa bendi hiyo inanyimbo nzuri ambazo zitamfurahisha kila mtu

Hii ni bendi ya tatu kuzinduliwa ndani ya jiji la arusha kwan kabla ya hii kipindi cha mwaka uliopita 2016 bendi mbili zilianzishwa jijini hapa ambapo bendi ya kwanza ya mjengoni  music band ilizinduliwa na pia kuna bendi ya East Afrika music bandi zote zikiwa ni bendi za musiki wa dance hivyo wakazi wa jiji hili wamenufaika kwa kuletewa music karibu tofauti  na kipindi cha nyuma ambapo wakazi wa jiji hili walikuwa wakipata tabu sana kupata burudani ya muziki wa live bandi .
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO