Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KINANA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM WILAYA YA MONDULI, MKOANI ARUSHA, NDUGU JACOB NKOMOLA, LEO JIJINI DAR ES SALAAM







































Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo ameongoza mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Jacob Nkomola, yaliyofanyika Mtoni Kijichi, Temeke Dar es Salaam.

Katika mazishi hayo walikuwepo piaa viongozi wengine wa ngazi ya juu wa CCM, wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu. Ngemela Lubinza.

Nkomola ambaye alifariki juzi jijini Dar es Salaam, mwili wake ulitangulia kuagwa nyumbani kwake, Mtoni Kijichi na baadaye kupelekwa katika Kanisa la Kianglikana, Mtoni Kijichi kabla ya kuzikwa katika makaburi yaliyopo Kijichi  saa kumi jioni. Kuona mfululizo wa picha tangu kuagwa mwili hadi maziko, tafadhali ingia CCM CHAMA BLOG/>BOFYA HAPA
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO