Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA wamshukia Ole Sendeka

*Wadai ameshindwa kuwatetea wananchi wake
*Yawahimiza wananchi kutoa maoni Katiba mpya

SAM_3006 WIMBI la mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) linaloendelea kwa kuendesha mikutano mbalimbali nchini, safari hii limemshukia Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM) na kumfananisha na ‘tikitimaji’.

Katika mkutano huo, ambao ulihutubiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho ambaye pia alikuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Arusha (UVCCM), James Ole Millya, walimlaumu ole Sendeka kuwa ameshindwa kupeleka maendeleo katika Jimbo lake, tofauti na maneno anayotoa.

Katika mkutano huo, Chadema walitumia usafiri wa helikopta (chopa), ambayo ilionekana kuwa kivutio kwa wakazi wa Simanjirio na vitongoji vyake.

Akihutubia mkutano huo, Lema alisema Sendeka amekuwa ni mtu ambaye hana msimamo kutokana na kulalamikiwa mara nyingi kuwa anapenda sera za Chadema.

Alisema tabia hiyo, ndiyo inayomfanya ashindwe kutetea maslahi ya wananchi wake, ambao wengi wanaishi kwenye lindi kubwa la umaskini, ikiwamo kukosa huduma muhimu za barabara, zahanati, elimu, afya na maji safi, licha ya utajiri wa madini uliopo.

“Leo jimbo hili halina maji, inasikitisha, hasa wananchi waliponiambia maji hayo ndiyo wanayoyatumiwa kwa ajili ya kunywa kutoka kwenye kisima wanachochangia na mifugo… hii ni hatari sana kwa afya zao, hakika hili halitakiwi kuwepo katika eneo hili ambalo wananchi wake wanaishi kwenye utajiri mkubwa wa madini aina ya Tanzanite,” alihoji Lema.

Lema aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao kwenye vikao vya Tume ya kukusanya maoni ya Katiba pindi itakapofika maeneo yao.

Alisema kama Katiba mpya, itafanyiwa marekebisho na kuondoa utaratibu wa kuondoa wakuu wa mikoa na wilaya ambao hulipwa fedha za umma, watakosa kazi za kufanya.

SAM_2870 Kwa upande wake, Millya aliwataka wananchi wa Simanjiro kuungana naye kwa kuhamia Chadema ili waunganishe nguvu katika harakati ya kudai haki zao, ikiwemo kunufaika na madini ya Tanzanite, yanayopatikana ndani ya wilaya hiyo.

Aliwataka wasitishike na vitisho wanavyotolewa na baadhi ya viongozi wa Serikali wa eneo hilo, ambao walitaka kuwazuia wananchi wasijitokeze kwenye mkutano wao.

Aliwataka wananchi hao kuwapuuza wale wote wanaojaribu kuwagawa kwa kigezo cha wenyeji na wakuja, kwa kile alichodai ni lengo la watu wasiolitakia mema taifa hili.

Viongozi wengine waliohutubia kwenye mikutano hiyo ni pamoja na aliyekuwa diwani wa Sombetini kwa tiketi ya CCM, ambaye hivi karibuni alihamia Chadema, Alphonce Mawazo na aliyekuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa CCM na UVCCM, Ally Bananga.
Katika mkutano huo, wanachama 1,200 kutoka CCM, walijiunga na Chadema.

Wanachama hao wa CCM, walirudisha kadi pamoja na sare za chama hicho, zikiwemo fulana, bendera na vitambaa vya kichwa katika mikutano iliyofanyika kwenye maeneo ya Narekauo, Lolbosiret, Naberera, Ndovu, Orkesument na Marerani

SAM_2935

Source: Mtanzania Picha zote na Tumainiel Seria

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO