Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mbowe: Mnyika, Lema na Dr Slaa watishiwa kuuwawa na kigogo wa Serikali

*Wadai ni mkakati wa kuwamaliza kisiasa
*Mbowe asema wamekuwa wakifuatiliwa kila kona waendako
*Kigogo wa Serikali adai hizo ni propaganda za kisiasa tupu

viongozi chadema

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana kuhusu madai ya baadhi ya viongozi wa chama hicho kutishiwa kuuawa. Wengine kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa; Mkurugenzi wa Mawasiliano, John Mnyika; na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Godbless Lema. (Picha na Deus Mhagale – Gazeti Mtanzania)

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeibuka na tuhuma nzito kuwa kuna mkakati unaofanywa na viongozi wa Idara ya Usalama wa Taifa, kutaka kuwaua viongozi wake kama njia ya kudidimiza harakati za chama hicho mbele ya Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alidai Serikali inatumia maofisa wake ambao wamefikia hatua ya kutoa vitisho kwa viongozi wa ngazi wa chama juu ya uhai wao.

Aliwataja viongozi ambao, wamekuwa wakitishwa kuuawa kuwa ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbles Lema.

Alisema kutokana na taarifa mbalimbali ambazo wamekuwa wakizitapa tangu Mnyika aliposimama bungeni na kutoa kauli kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, ni amekuwa akifuatiliwa ndani na nje ya Bunge, huku akipokea vitisho vya kuuawa.

“Mnyika, alisimama na kutoa kauli juu ya udhaifu wa Serikali bungeni, sasa imeonekana nongwa hata kufikia kutishiwa maisha yake pamoja na Dk. Slaa, jambo hili tunasema ni hatari kwa viongozi wetu.

“Kwa mujibu wa vyanzo vyetu kutoka ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa, vinaeleza kuwa mpango huo, unaratibiwa na kiongozi mkubwa (jina tunalo) na ofisa mmoja anayefahamika kwa jina la Rama. Hawa kila wakati wamekuwa wakifuatilia nyendo za viongozi wetu, ikiwemo kutoa vitisho dhidi yao.

“Kutokana na hali hiyo, tumelazimika kuitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu kesho (leo), ili kujadili kwa kina suala hili na moja ya ajenda, itakuwa ni hali ya vitisho kwa viongozi wetu,” alisema Mbowe.

Alisema chama chake hakitarudi nyuma kupigania haki za Watanzania pamoja na kupokea vitisho hivyo.

Alisema kutokana na hali hiyo, kumekuwa na kugeuza ajenda ya mgomo wa madaktari na kukinasibisha chama chake hali ya kuwa hawahusiki na kuwaambia madaktari kugoma kama inavyodaiwa na baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndani ya Bunge.

Kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea, alisema Serikali inapaswa itafakari upya uamuzi wake kwa kukaa pamoja na madaktari, ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu, kuliko kuwafukuza.

“CHADEMA haikuwaambia madaktari wagome na wala haihusiki na mgomo wao…. ila tutakuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya kila kundi kwa mujibu wa utaratibu uliopo,” alisema

Chanzo: Mtanzania, 09 July, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO