Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Uchaguzi Naibu Meya Arusha leo

Hatimae baada ya mgogoro wa nafasi ya unaibu meya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Arusha kudumu kwa muda mrefu, uongozi wa hamashauri hiyo umeamua kuitisha uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo.

hii ni mara ya tatu kwa uchaguzi wa nafasi ya unaibu meya kuitishwa na hamashari hiyo ambapo itakumbukwa kwama uchaguzi wa kwanza ulifanyika mwaka juzi baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa naibu meya wa jiji hilo, Michael Kivuyo ambae pia ni diwani wa TLP.

Uchaguzi wa pili wa nafasi ya naibu meya ulifanyika mwaka jana baada ya baadhi ya madiwani wa CCM na CHADEMA kuingia mwafaka wa kutatua mgogoro wa umeya wa jiji hilo ambapo diwani wa Kata ya Kimandolu, Estomi Mallah alichaguliwa kushika nafasi hiyo ambapo baadae yeye na wenzake wanne walitimuliwa na kisha kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu ya CHADEMA.

Taarifa zilizopatikana mjini hapa zilisema tayari uongozi wa manispaa hiyo umeshawaandikia barua na kuwakabidhi madiwani wote kuwajulisha kuhusu ratiba ya uchaguzi huo ambao utafanyika leo na kesho.

hata hivyo, habari hizo zimedai kuwa uchaguzi huo umepingwa vikali na madiwani wa Chadema kwa madai umekiuka taratibu na kanuni za kudumu za halmashauri hiyo.

Taarifa hizo zilienda mbali zaidi na kusisitiza ya kuwa tayari Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema jijini hapa, Isaya Doita ambae pia ni diwani wa Kata ya Ngarenaro ameuandikia uongozi wa manispaa hiyo barua nzito ya kupinga uchaguzi huo kwa madai kuwa umekiuka taratibu kwa kuwa wamepewa taarifa katika muda usiostahili

Sababu nyingine ya diwani huyo kupinga uchaguzi huo ni kulalamikia kitendo cha manispaa hiyo kushindwa kuvitaarifu vyama husika ilhali ndivyo vyenye dhamana ya kuteua wagombea wa nafasi hiyo.

BOFYA HAPA kujionea jinsi uchaguzi wa Meya wa Manispaa hiyo ulivyokuwa

Source: Moses Mashalla, Mwananchi 10 July, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO