Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

FILAMU YA "SAYLA” KUZINDULIWA KESHO NAURA SPRING HOTEL-ARUSHA, WAIGIZAJI NIA PAMOJA NA ZITTO,HALIMA MDEE, SHY ROSE BHANJI

Filamu ya SAYLA inayozungumzia nmana watanzznia walivyoweza kumsaidia Sajuki kupata matibabu inatarajiwa kuzinduliwa mjini Arusha kesho Julai 13, 2012 katika hoteli ya Naura Spring kwa kiingilio cha Shs 20,000 kwa siti za VIP.

Baadhi wadau na wasanii waliocheza filamu hiyo ni pamoja na Wema Sepetu, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya.

Wengine ni Mbunge wa Kawe, (CHADEMA), Halima Mdee, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, (CHADEMA), Zitto Kabwe, watangazaji maarufu, Maimatha Jesse, Ephraim Kibonde na wengineo.

Kwa mujibu wa maelezo ya msanii  Wastara Juma, mhusika mkuu katika filamu hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Dunamic Minds ni Angela Karashani.

Wastara ambaye ni mke wa muigizaji, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amewashukuru Watanzania kwa msaada wao wa hali na mali na kuwataka wamuunge mkono katika ununuzi wa filamu hiyo, ambayo mapato yake yatakwenda katika kumsaidia Sajuki na familia yake kwa ujumla.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO