Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MwanaCHADEMA Arusha ashitaki kutishiwa maisha na wanachama 5 wa CCM

DSCN9804

Hassan Noor akiwa na mtoto wake anaeonekena kurithi nyendo za baba yake katika siasa

Mwanachama machachari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kata ya Kati Jijini Arusha, Bw Hassan Noor (pichani) jana amefungua Jalada la malalamiko kaitka Kituo Kikuu cha Polisi Arusha kulalamikia watu watano wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa mjini hapa kumtishia maisha kwa maneno makali na kuahidi kumfanyia jambo baya ambalo hawakulitaja.

Noor amefungua shauri hilo katika kituo hicho cha Polisi na kusajiliwa kwa RB No. AR RB/8258.

Leo Jumaane, mmoja wa watu hao ambae emetambulika kwa jina moja tu la Bw Mbezi amekamatwa na Polisi na kufikishwa kituoni hapo, baadae akaachiwa kwa dhamana.

Mlalamikaji anahitajika kuripoti kituoni hapao kesho asubuhi kwa hatua zinazofuata.

Haijaweza kuthibitika sababu hasa za watu hao kumtishia maisha mwenzao lakini kwa mujibu wa maelezo ya mlalamikaji ni sababu za kisiasa.

Noor ambae amejizolea umaarufu katika mitaa ya katikati ya Jiji, hususani eneo la Kata ya Kati jirani na Mgahawa wa Revolution, kwa kutumia vazi la khaki ‘kombati’  muda wote awapo kazini, ameeleza kuwa hali hiyo imemfanya kuwa na maadui wengi wengine wakiwa marafiki zake ambao wamejaribu kumshawishi aachane na CHADEMA akawakatalia.

Kwa maelezo ya wanaomfahamu Bw Noor , wanasema anonekana kuwa kiungo muhimu sana kwa chama chake jambo ambalo halijawapendeza wengi ikizingatiwa kuwa eneo hilo ndio sehemu pekee ambayo inaonekana bado kuwa ngome ya CCM katika Jiji hili.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO