Juzi Jumamosi July 7, 2012, kamanda mpya wa CHADEMA ambae awali alikuwa Kiongoziwa Vijana (UVCCM) Arusha Ndg Kames Ole Millya aliambatana na makamanda wengine wa chama hicho kwenda Wilayani Simanjiro kusambaza ujumbe wa Vuguvugu la Mbadadiliko (M4C) kwa jamii ya maeneo hayo.
Mapokezi ya ujumbe wa Millya katika vijiji tofauti tofauti alivyotembelea yalikuwa ni ya furaha tupu ikiwa ni sambamba na kuchinja ng'ombe 7 na kuchoma nyama, kurukaruka na kuimba nyimbo za kitamaduni (Maasai culture)
Zifuatazo ni taswira za matukio tofauti ya ziara hiyo katika vijiji tofauti
Picha juu, Millya (mwenye kombati) anazungumza na mzee wa kimila mara baada ya kuwasili jijiji cha Olubousoieti. Picha chini ni baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea kijijini hapo.
Zoezi la uchomaji nyama linaendelea..ililazimu kikosi kazi kuweka kambi mahali hapa kuweza kusubiria kitoweo hiki.
Wazungu nao wakaunga msafara kula nyama porini..
Nyama zilikuwa tamu sana. Mwingine mwenye kombati ni kamanda mwingine wa chama hicho toka Same, Ndg Christopher Mbajo
Hapa Millya akifafanua masuala mbalimbali kwa wananchi wa Simanjiro
Morani wa kimasai “wakipandisha mori” kitamaduni zaidi
Wakati wa kurudi, msafara wa Millya ulilazimishwa kusimama na kupewa supu kabala ya kurudi mjini
0 maoni:
Post a Comment