Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA wazidi kujiimarisha maeneo ya wafugaji wa Kimasai; taswira za ziara ya chama Kata ya Ruvu-Muungano, Same

DSC04224 Ally Bananga aliewahi kuwa mjumbe wa NEC CCM akiwakilisha vijana wa Arusha, akihutubia wananchi wa eneo la kijiji cha Marwa, Kata ya Ruvu Muungano Wailayani Same katika ziara ya chama chake kipya cha CHADEMA. Banaga na wanachama wengine walilazimika kusimama kijijini hapo kuzungumza na wananchi kwa muda baada ya kushindwa kufika eneo la Nesuriet lilipo katika Kata hiyo kutokana na kuchelewa kulikosababishwa na ubovu wa barabara. Awali ilipangwa kuwa watafanya mkutano mkubwa sana eneo la Nesuriet, mkutano mabao wenyeji wao waliandaa mbuzi kadhaa. Pamoja na kushindwa kufanikisha mkutano huo, viongozi na makamnada hao wa chadema watazuru tena eneo hilo wiki ijayo ili kutowakwaza wenyeji wao waliowasubiria sana.

DSC04210 Diwani wa Moshi Mjini (CHADEMA) Mh Hawa akizungumza na wananchi hao

DSC04163 Ishaya ya mwitikio wa “Peoples Power”

DSC04168 Bananga (alieweka mikono mfukoni) akijadiliana jambo na wanachama wengine walioambatana nae katika ziara hiyo kabla ya kuzungumza na wananchi, wote wanatokea Arusha. Mwenye shati jeupe ni Christian Mbajo, mwenyeji wa Same lakini shughuli zake ziko mjini Arusha.

DSCN4705Wananchi walihamasika sana, juzi Jumapili Julai 15, 2012. Wadada wawili wanoonekana kama mabodigadi wa Mh Hawa ni wanachama wa Baraza la Vijana wa chama hicho Mkoani Kilimanjaro.

DSCN4719 Wakizuru makazi duni ya wananchi hao

DSCN4775 Diwani Hawa (CHADEMA) katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa CHADEMA kitongoji cha Marwa (mwenye skafu) na mke wake

DSCN4793

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO