Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kamati Kuu CHADEMA kukutana kwa dharura leo kujadili tishio la kutaka kuuwawa viongozi wao

Kamati Kuu ya Chama che Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inakutana leo kwa dharura ili kujadili kwa kina suala la hali ya vitisho kwa viongozi vya chama hicho.

Mwenyekiti wa chama hicho, Mh Freeman Mbowe alitangaza uamuzi ho wakati akizungumza wa waandishi wa habarai jana kuelezea taarifa alizodai kuzipata zikihusisha mpango wa kuwadhoofisha kisiasa kwa kupanga njana za kuua viongozi wa chama chake kwa kuanza na Dr Slaa, Mnyika na Lema.

******

Ifuatayo ni sehemu ya bandiko lililopatikana katika mtandao wa Jamii Forum jana, likionekana kutoka kwa mmoja wa viongozi au amtu alie karibu na viongozi wa chama hicho lenye kichwa cha habari “TUHUMA nzito kwa UWT/TISS; CHADEMA yabaini njama nzito kumaliza viongozi wake”

“Wakuu habari za Jumapili

We have just finished a Press Conference here at HQ, ambapo kutokana na uzito na umuhimu wa suala lilizongumzwa leo mbele ya wanahabari, viongozi wakuu wa chama, Mwenyekiti Taifa Kamanda Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dkt. Willibrod Slaa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Musa Hamad Yussuf, baadhi ya wakurugenzi na maofisa wa makao makuu walikuwepo.

Kwa kifupi. Walau kwa kuanzia sasa; CHADEMA kimeshusha tuhuma nzito kwa serikali, hasa Usalama wa Taifa kuwa wanapanga njama za kutaka kuwamaliza kwa mbinu mbalimbali, zikiwemo za kutumia sumu, kijambazi (kutesa) na zingine, viongozi wa CHADEMA, ambapo kwa kuanzia tayari mkakati unaandaliwa kuanza na John Mnyika, kisha afuate Dkt. Slaa na baadae Godbless Lema.

Baadhi ya watu wa TISS wametajwa kwa majina wakituhumiwa kuhusika katika njama hizo ambazo tayari watu wameshawekwa kuanza kazi rasmi.

Naibu Mkurugenzi wa UWT, Zoka ametajwa kuwa katika njama hizo, ambapo tayari kikosi kinachoongozwa na mtu anayeitwa Rama kimetumwa Mjini Dodoma kuanza harakati za namna ya kummaliza John Mnyika, kisha wengine wafuatie.

The whole story is coming...
Hasa njia wanazopanga kutumia kutekeleza mpango huu wa hujuma ya kikatili dhidi ya fikra huru zinazopigania mabadiliko ya kimfumo na kiutawala.

Another serious show down to justify how the failing, falling and collapsing government behave towards its people. As Chairman Freeman Mbowe has put it "Rule of Terror" – mwisho wa kunukuu!!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO