Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Breaking News: Meli yazama Zanzibar

seagull4 Meli ya Mv Seagull ikiwa na abiria zaidi ya 200 ikotokea Dar es Salaaam kwenda Zanzibar inasemekana kuwa imezama (Picha kwa hisani ya Daily Mitkasi Blog)

Meli iliyokuwa imewabeba takriban watu miambili imethibitishwa kuzama katika Bahari ya Hindi eneo la Chumbe kisiwani Zanzibar. Meli hiyo kwa jina SKAGIT ilikuwa inatoka Dar Es Salam kuelekea Zanzibar.

Kulingana na taarifa za vikosi vya wanamaji , meli hilyo ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali.

Jeshi la polisi la wanamaji nchini Tanzania limeanza shughuli za kuwaokoa watu zaidi ya mbia mbili wanaohofiwa kuwa kwenye meli ya Skagit inayoripotiwa kuzama huko visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, ingawa hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo, lakini wamethibitisha kwamba meli hiyo imepigwa na dharuba ya upepo mkali katika eneo la Chumbe pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam kuelekea visiwani Zanzibar.

Itakumbukwa kwamba, ni takriban mwaka mmoja sasa tokea ajali ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800

Source: BBC Swahili

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO