Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Wananchi waichambua hotuba ya Mh Peter Msigwa (Mb) aliyoitoa Bungeni Juni 19, 2012 akichangia mijadala

Hotuba na mchango wa Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mh Mch. Peter Msigwa katika Mkutano wa Nane, Kikao cha Tano – Tarehe 19 Juni, 2012 Bungeni Dodoma

Msigwa bungeni

Mh Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA)

Mh alitiririka kuanzia hapa…
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi.Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuanza kwa nukuuambayo naipenda sana inayosema:-

“Insanity is keeping doing the same thing in the same way and expecting different result”
ambazo zinalikabili taifa lakini kwa bahati mbaya nimeona yaani uwendawazimu nikufanya jambo lilelile kwa njia ileile huku ukitegemea matokeo tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanafalsafa Albert Einstein anasema:-“Problems can not be solved by the same level of thinking that creates them”.

Ndugu zangu, kabla sijawa Mbunge kama alivyosema kaka yangu Mheshimiwa Akunaay, nilikuwa nawa-admire sana Wabunge wanavyokuwa Bungeni, wakivaa suti, nilikuwa naona hapa ni mahali ambapo tuna reason, mahali ambapo tuna question na mahali ambapo tunatoka na solutions

is the opposite, binafsi najisikia vibaya sana. Kama taifa tupohapa, we are dealing na future ya taifa hili, tunashughulika namamia ya maskini wa Tanzania, tunashughulika na barabarambovu za Watanzania, tunashughulika na hospitali mbovu zaWatanzania, halafu tunakuja hapa tunaongea mambo yakhanga!

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma historia, nchi za Ulayakarne ya 14, Marekani na Ulaya na nchi zilizoendelea, zilikuwana fikra na mawazo kama tunavyofanya sasa hivi lakini ilipofikakarne ya 18, inaitwa age of enlightenment, reasoning age, walianza kufikiri, kuhoji na kudadisi. Tunapofika katika karne hiikatika Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania,tunapojadili bajeti maana yake tunazo changamotozinazotukabili kama taifa.

Badala ya kukaa na kujiuliza kwa ninitupo hapa, tunatokaje hapa tulipo, tunaanza kuongeangonjera na maneno ya uswahiliuswahili yaani unafiki, woga,kujipendekeza na kutokujadili mambo ya msingi.
(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najisikia uchungu sana mamiaya wananchi wametuamini tuje tujadili vitu vya maana hapalakini tunakubaliana akili ndogo itawale akili kubwa. JamesMadison mwaka 1822 alisema, “
knowledge forever will governignorance”.

Tumekubali Bunge hili knowledge ndogo i-governknowledge kubwa, tumekubali ignorance i-govern knowledge,tunalipeleka wapi taifa?

Akichangia professor hapa hanatofauti na mtu wa darasa la pili. Huwezi kutofautisha mtumwenye masters na mtu wa darasa la pili, where are we takingthis nation? Watu wametupa kura, tunapoteza fedha zaWatanzania, tumekaa hapa tunaacha kujadili mambo yamsingi kwamba tunawezaje kutoka kwenye matope haya?

Karne hiyo ya 18 ninayoisema walipoanza kuhoji, walipoanzakudadisi ndipo mapinduzi ya viwanda yalivyojitokeza, no wonder watu wanaosema ni wataalamu wa uchumi wametufikisha hapa tulipo, if that is the case, haya ndiyo masuala ambayo tunapaswa tuyajadili kama taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inaonyesha hapa, kitabu cha uchumi cha Mheshimiwa Wassira kwamba deni limekuwa shilingi trilioni 20. Ukigawanya ni kama karibu kila Mtanzania anadaiwa shilingi laki nne na themanini na zaidi, hata mimba inadaiwa, ndiyo taifa tulipofika hapa sasa hivi.

Pianinashangaa katika mpango wake wa bajeti taifa hili kamatunafuatilia na tunakwenda na takwimu, mdogo wangu amezungumza hapa kwamba tunatumia takwimu za nyuma, unawezaje kupanga mambo na takwimu za nyuma?

Leo hii katika taifa hili 44.2% ni watoto walio chini ya miaka 15 maanayake hawa ni consumers, wanakula zaidi hawa-produce, wakoshuleni na wanao-produce katika nchi hii ni wachache sanakuliko wanaokula ukijumlisha na wazee tuna mzigo mkubwasana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa utaratibu wabajeti tulio nao hapa,
there is no way kama tunaweza tukafanya maendeleo, it will take ages kubadilisha taifa hili kama tunaendelea na ngonjera za namna hii na kuruhusu akili ndogo itawale akili kubwa.

Watu wenye akili kubwawanaweka akili zao mfukoni kwa sababu ya ushabiki wakivyama badala ya kukaa tuka-discuss namna ya kutatuamatatizo yetu.Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama wanao-consume niwengi na wanao-produce ni wachache maana yake nini?

Tutaendelea kuomba fedha nje na kukopa fedha nje ilituwalishe kwa sababu ni wajibu wa Serikali kusomesha watoto,ni wajibu wa Taifa kuhakikisha watoto wanavaa na kusomashule nzuri lakini mpango mzima wa uchumi uko kimya,hauzungumzi.

Hapa watu wasomi ambao tupo 350 taifalimetuamini tukae hapa tunatakiwa tujihoji, ndiyo maananimesema problems can not be solved by the same level ofthinking that created them, you guys you are tired!

Kwasababu hamuwezi kutetea matatizo haya, mmetuwekakwenye mess ninyi wenyewe, ni lazima akili ya juu zaidi iwezekutatua, ni principle hii yaani huwezi kubadilisha that is theprinciple, iwe ni mwanamahesabu na nikiunganisha na insanityis keeping doing the same thing in the same way andexpecting different results and this is what we are doing.

Tunafanya hayohayo kila mwaka bajeti ya namna hiyohiyo.Ukienda kwenye elimu ni matatizo, ukienda kwenye kilimo nimatatizo, ukienda kwenye afya ni matatizo mwaka baada yamwaka ni matatizo yaleyale,
why can’t we think a little bitmore? We can’t stretch our brain a little bit more kama taifa?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeongea na watu wengineambao ni ma-professor wanasema mara nyingi wakitoaushauri wa kitaalamu, Serikali hamsikilizi na inawezekanawanakaa watu wachache, wanajifungia halafu wanatoamaamuzi kwa sababu wanajua mambo ni yaleyale, business asusual. Ndugu zangu, where are we going? Where are we heading?
165

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonyesha tenakaribu 42% ya watoto wanaozaliwa wanadumaa,
they can notthink properly, they can not question, they can not ask.

Ubongo aliotupa Mungu ni lazima uwestretched ili uwezekuchambua kwani tumeumbwa ili tutatue matatizo hapaduniani na siyo tu-create matatizo. Tulipokuja hapa Bungenitunatakiwa tu-solve problems, Bunge hili naliomba liwe Bungela kimapinduzi, tu-change namna ya kufikiri na tu-change namna ya kufanya vitu na wengine wanapata taabu hapakwa sababu tumezoea Bunge la chama kimoja.

Tuna mfumona traditional ya chama kimoja cha zamani, ulimwengu umechange halafu tumesimama mahali pamoja hatuendi naulimwengu unavyokwenda. Maendeleo duniani yamekuja kwakuwa na mawazo tofauti yanayopingana, badala yakutuzomea mtusikilize, huu ndiyo wajibu wetu. Mimi kama opposition siwezi kusifia bali nakukosoa ili ufanye kazi yako vizuriili na wewe utimize wajibu wako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa deni kama hili kila mwakalinaongezeka halafu tunakaa hapa tunasema Serikali ya CCMitaendelea kutawala, so what? Ili iweje? Kwa sababu lengo la Serikali kuwepo ni kutatua matatizo ili tuhakikishe tuna-improve maisha ya watu lakini watu kwa sababu wanalinda vyeo, kunammoja amesema Mchungaji, lakini nitasema tu hata kamamtasema au kunitoa nje ya Bunge lakini kama ukweli unakosewa

I will speak out kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya Wachungaji vilevile. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mbunge mmoja alishaurihapa tuombewe lakini sioni hata theory ya uchumi inayosemakama unataka kutatua matatizo ya uchumi eti ufanyemaombi, ninashangaa huyu amepata wapi hilo?

As aTheologians hata Paul anasema asiyefanya kazi na asile siyo aombewe, unamnyima chakula lakini yeye anasema watu waombewe. Mimi kama Mchungaji naombea wazinzi, wanaofumaniwa na wake za watu, ndiyo tunawaombea, mimi kama Mchungaji tunawaombea wenye mapepo na hii ni principle tuna apply, una-consumers wengi lakini producers wachache maana yake you have to produce more tafuta njiaza ku-produce zaidi, we don’t pray for this, we don’t have topray for this. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu tumekaa hapatumezalisha taifa la watu waoga, wanafiki nawanajipendekezapendekeza, mimi sijaja hapa kwa kupewafedha bali wananchi wa Iringawamenichangua, wananiaminina ninajua wananiunga mkono, wananisikiliza. Sasa sihitajikujipendekeza nitaeleza ukweli as a nation tupo kwenyematatizo. We have to address this problems lakini siyo tunakujahapa tunaweka ngonjera maneno ya khanga halafu watumnawapigia makofi, tunalipeleka wapi taifa hili? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajisikia uchungu, naomba
niachie hapo. Ahsante sana. (Makofi)

********

Hotuba hii imepetikana kupitia mitandao ya Kijamii kama Facebook n.k.

Miongoni mwa wananchi waliotoa maoni yao kuhusiana na hotuba hiyo ni hawa hapa..

  • Ado Marley dah...unaweza kulia kwa kuona taifa linaenda mrama kiasi gani...inshallah...time heals! 2015 is our time to make changez

    Jacob Edwin Ntundu KaoNGEA SANAX LAKIN NA YEYE KAWEKA POROJO CJAONAX HATA SOLUTIONX ALIYOTOA APO ZAIDI YA KUQUOTES MISEMO YA WANAPHILOSOPY NDO YALEYALE MANENO MENG MAZUR HAKUNA SULUISHO WE KEEPIN ROUNDING THE CYCLE...KABARIKIWA KUONGEA MANENO YA HAMASA KANYIMWA UWEZO WA KUTOA USHAURI WA KUTATUA MATATIZO NDO WANASIASA WETU HAO

  • GEng Ester Christopher Mwabulwilo ni kweli ana uchungu lkn bado ni siasa je tunaweza kupima matokeo ya hotuba yake? saizi tunahitaji mtu aongee kitu measurable and deliverable.

  • Denis Nzowa steve tunahitaji wabunge 5 tu kama mch. msigwa kwan 10 ni weng xana, ndo wanastahili posho ya laki 2 na huo salary ya milion kadhaa, duu ripot yake imenikuna ngoja niisave baadaye nisome tena, myself nampa uspika kivuli.

  • Albert Mngulu Nimeisona kwa kina na nimependa alichoongea..tatizo wabunge yanaingilia sikia ili na kutokea sikio la pili..big up Msigwa..

  • Musa Kumondawa Kajitahd kuongea bt hajatoa way forward! So bdo kidogo ila kajitahd sana kueleza ukwel

  • Abiud Laurent Yap steve wabunge wa namna hiyo ndio majembe iringa walichagua mbunge wanastahili hongera
    Steven Mwakyusa Mpaka akili ndogo itakapoacha kuongoza akili kubwa ndipo...ndipo hizo way forward zitakapofanya kazi...kwa mwenye kufikiri sawa sawa...hii ni zaidi ya shule

  • Musa Kumondawa Jaman hebu 2jaribu kuwa waelewa kidg, hata hata maongez ya Mh. Msigwa yana2shinda kuelewa lengo lake,,, kama mmesoma vzur hiyo doc anachojaribu kukilenga Mh. Ni kwamba wabunge wengi wanaongea mambo yasio ya kimsing wengne wanaongelea ushabk na kujipendekeza kwa hiyo anajaribu kutoa DIRECTION ni mambo gani ya msing yaliyowapeleka pale mjengon ili yaweze kujadiliwa na kutafutiwa soln,,,, alichokifanya Mh. Msigwa ni kusaidia kuwaweka wabunge wenzake ktk mstar sahh ili waweze kugundua ni mambo gani muhm ya kujadiliwa na kuweza kuyapatia soln na c kutoa soln ya hayo mambo..... Habar za macku mengi wadau wenzangu??? Am back again

  • Abbas Hussein Kama ni prof basi atakuwa sawa na mwanafunz wa darasa la pili... Sasa kama hana hata masterz cjui Abbas Hussein Namkubal sn huyu Mh. Kwa kwel wana Iringa 2nawashukur kwa ku2zalia mashujaa namkumbuka sana Mkwawa, wazungu hawana ham nae hata chembe, kudadadek.....

  • Elias Ezekia Mwakapimba Mnaochangia humu na kumbeza Mch. Msigwa nina wasi wasi na uelewa wenu. Amesema ameongea na maprofessa ambao wengi wamelalamika ushauri wao hausikilizwi na serikali ya NYINYIEMU. Sasa mnataka Msigwa apoteze muda kuishauri mijitu, migwiji ya ufisadi, Magamba isiyoshaurika?
    Wana wasomi daraja la kwanza wanataka tuwaombee, au nanyi humu ndani tuwaombee!
    Ushauri mwingi katoa, ambao kwanza ni kuwabadilisha Magamba namna ya kufikiri. Unataka magamba walishwe bisi wakati ndo kwanza wanakatwa vitovu (umbilical cord)? Be analytical.

  • Elias Ezekia Mwakapimba Way forward kubwa kasema, waondoke madarakani. Rudia kusoma uelewe vizuri wewe unaebeza

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

Anonymous said...

This is our time for revolution tz.we need changes! Who can make changes? It's u. Ukweli uko wazi ndani ya Nchi yetu ni kwamba wenye dhamana ya kututawala wameshindwa sasa ni wakati wetu,yaani mm na ww.hakuna kitu kibaya kama mtu kukufanya mjinga wakati una akili yako na hakuna kitu kibaya kama kupokonywa mali yako na huku unaona na ukitaka kuzuia mlinzi wako anakuonyooshea silaha, tena ulio mnunulia ww.nafikili wengi tunaupeo sasa wakuona na kutambua kipi kizuri na kipi kibaya.eewe mtz mwenzangu tuungane tuokoe taifa letu hawa jamaa hawana machungu nalo walikuwa wana msubili mchonga alale ili wao waamke ndo kama hivi unavyoona.

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO