Profesa Lipumba ambae ni Mwenyekiti wa CUF Taifa na pia kiongozi wa jopo la wachumi Duniani akizungumza na waumini wenzake wa dini ya Kiislamu (hawaonekani pichani) Mjini Arusha jana.
Sehemu ya Jukwaa kuu maalumu kwa viongozi waalikwa
Sehemu ya waumini waliohudhuria viwanjani hapo wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakiislamu jana katika viwanja vya msikiti wa Ijumaa, Kata ya Kati mjini Arusha.
(Picha zote na Tumainiel Seria)
**********
PROFESA Ibrahimu Lipumba jana alipata nafasi ya kuzungumza na waumini wa dini ya Kiislamu Mjini Arusha, katika viwanja vya Msikiti Mkuu wa Ijumaa Kata ya Kati ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka waumini hao kujitokeza kwa wingi kutoa maoni na mapendekezo yao kwa Tume inayokusanya maoni ya wananchi kuandika Katiba mpya.
Akizungumza katika mkusanyiko huo uliokuwa na agenda kuu tatu; Sensa ya watu na makazi, Mchakato wa Katiba mpya na Haki za waislamu nchini, Profesa Lipumba alisema kwamba anawasiwasi na muda wa miezi 18 kama utatosha kuweza kukusanya maoni ya wananchi kwa mawanda yanayostahili.
Lipumba alisema kuwa Taifa linahitaji Katiba ya Kidemokrasia ambayo itatambua uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi tofauti na iliyopo hivi sasa ambayo alidai haiko huru na haitendi haki.
Alisisitiza umuhimu wa Tume hiyo kuundwa mapema kwa vile mchakato wa kupata Katiba mpya umekwisha anza, na kueleza kwamba enadapo maoni yatakusanywa na kisha wananchi wakapiga kura ya maoni wakakataa ni wazi kuwa mwaka 2015 uchaguzi utafanyika kwa kutumia Katiba ya sasa jambo ambalo alidai linaweza kuleta hali tete nchini.
“Swala la Tume huru lazima lipewe kipaumbele. Ikiwa tutasubiri mchakato wa uchaguzi ndio tuanze mchakato wa tume huru, tukienda na mfumo wa Tume iliyopo 2015 itakuwa kasheshe” alisema Prof Lipumba.
Prof Lipumba aliwataka waumini hao kutoa maoni yao kwa uhuru na hoja zinazolihusu taifa na raia wake na kusisitiza kuwa mawazo yasisitize umuhimu wa kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya watu wote.
Akigusia swala la Mahakama ya Kadhi, Profesa Lipumba alisema hiyo ni haki ya kimsingi kwa waislamu na kuitaka Serikali kuondoka woga wa kuruhusu uwepo wa mahakama hiyo nchini.
Aidha, viongozi waliopata kuchangia awali kabla yake waliktumia sehemu kubwa ya hotuba zao kusisitizia maswala ya haki za waislamu ambazo walidai ni kama vile wananyimwa ka makusudi na kuwapendelea watu wa imani nyingine.
Bila kufafanua zaidi, viongozi hao waliwataka waumini hao kuungana ili kuhakikisha uchaguzi wa 2015 wanahakikisha wanatumia nafsi hiyo kuchagua watu ambao watatetea maslahi yao ambao kwa mujibu wa hotuba hizo hawapaswi kuwa watu wa chama fulani cha upinzani ambacho kimekuwa mwiba kwa Serikali hivi sasa (jina linahifadhiwa).
Wakizungumzia swala la sensa ya watu na makazi inayaotajariwa kufanyika mwezi ujao kote nchini, viongozi hao wakiimani waliwataka waumini wote wa Kiislamu kususia zoezi hilo la sensa hadi hapo watakapo jua wako waislamu wangapi nchini kwa maelezo kwamba mara zote wamekuwa wakihesabiwa lakini hawaambiwi idadi yao.
0 maoni:
Post a Comment