Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Wananchi wa Muriet Kata ya Sokoni-I Arusha wailalamikia Manispaa kutaka kuwadhulumu fidia ya viwanja vyao kupisha upanuzi wa dampo

Manispaa ya mji wa Arusha inalalamikiwa na baadhi ya wananchi ambao hawajaridhika na zoezi la fidia kwa mali zao kuafuatia uamuzi wa Halmashauri ya Manispaa kutaka kupanua na kuboresha dampo la takataka lililopo eneo la Muriet kuwa la kisasa zaidi, sambamba na uboreshaji wa maeneo mengine ya mji katika mpango wa Kuihuisha Ardhi kwenye maendeleo ya kimji.

Siku ya Juni 30, 2012 wananchi wapatao 65 walikusanyika eneo la dampo hilo, wote wakiwa waathirika wa zoezi la fidia kwa nyumba na mali zao ambazo zinapaswa kubomolewa kupisha upanuzi wa dampo kwa kiwango cha mita 100.

Wakizungumzia historia ya mgogoro huo wanasema, hapo awali ilikuwa nyumba zao zibomolewe kwa eneo kubwa zaidi nao wakapinga lakini baadae kukawa na maafikiano kuwa ubomoaji utawahusu walioko ndani ya mita 100 tu tena kwa klipwa fidia.

Wanalalamikia kutoshirikishwa kwa uwazi katika zoezi la tahmini ya mali zao. wanadai kuwa waliletewa tu karatasi na kuelekezwa mahali pa kusiani bila kufahamu fedha wanazosaini zinauhalali gani na thamani halisi ya mali.

Baadhi walidai kuwa kuna ambao wameshasini na wengine wamekataa. kati ya watu 48 waliofanyiwa tathmini, watu tisa wamegoma kutia saini kwa madai kwamba fidia waliyopangiwa hailingani na thamani halisi ya mali zao, na pia wanapinga kitendo cha wenye viwanja visivyo na kitu kutohesabika katika zoezi hilo la fidia.

Kwa mfano, Mzee Raphael Saitoi alieleza kushangazwa na mtu mmoja kuandikiwa fidia ya sh mil 30 na mwingine wa eneo hilo hilo mwenye mali karibu zinazolingana kuandikiwa sh mil 2 tu, na wengine chini ya hapo.

Saitoti alienda mbali zaidi na kueleza wasiwasi wake kuwa huenda kuna njama za watendaji fulani katika Halmashauri hiyo wana njama za kutaka kujineemesha wao kwa njia za kifisadi kupitia sthaiki halali za wananchi.

Akifafanua zaidi, alitolea mfano wa barua waliyopewa kufuatilia fidia mbayo haina logo ya manispaa, haina mhuri wa manispaa wala tarehe na kumbukumbu namba lakini ikiwa imesainiwa na Afisa Ardhi Mteule, Ndg Kiwera M. Kiwera

Maswala mengine yaliyoibuliwa katika mkutano huo ni pamoja na kupinga kitengo cha Manispaa ambao ni washitakiwa katika kesi waliyofungua siku za nyuma kuhusiana mgogoro huo, Land Case No. 4/2008, kufoji barua ili kuonesha kuwa kulikuwa na makubaliano baina ya halmashauri na wananchi hao kufuta keso yao ili wamalize kwa mazungumzo nje ya mahakama.

Wananchi hao kwa pamoja walionesha kusikitishwa na kitendo hicho na kukilaani vikali huku wakikanusha kuwa hakuna kikao kilichowahi kukaa wakakubaliana kufuta kesi yao.

Swala hilo lililamlazimu mwanasheria aliealikwa kuwasikiliza, Ngd James Lyatuu kueleza kwamba kwa taratibu za kimahakama mshitaki ndio huwa anaepswa kufuta shauri na sio mshitakiwa kama ambavyo Manispaa imefanya.

Hatimisho la kikao hicho ilikuwa ni muafaka wa pamoja kupeleka zuio Mahakamani ili utekelezaji wa zoezi la ubomoaji lilikuwalimepangwa kuazna July 2, 2012 kusimama kwa muda hadi hapo muafaka wa pamoja utakapopatikana ikiwa ni pamoja na kuifufua kesi yao ambayo wanadai imefutwa kihuni tena kinyume cha taratibu.

DSCN4397 Hawana ndio wananchi ambao bado wana malalamiko na fidia kwa nyumba na mali zao. watu 9 miongoni mwao wamegkataa kusaini fomu za fidia ili nyumba zao zibomolewe kwa madai kwamba fidia husika hailingani na thamani halisi ya mali.

DSCN4374 Ndg Burkady Kalist “Bush” akifafanua jambo wakati akizungumza na wananchi wa Muriet wanaopinga zoezi la fidia kupisha upanuzi wa dampo. Kalist aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho kupitia TLP kwa miaka 10 kabla ya kuamua kuhamia CHADEMA hivi karibuni. Bado wananchi wanakumbuka mchango wake maana ndio alisaidiana nao kupinga ubomoaji wa awalai ambao ilikuwa ufanyike bila fidia yeyote. hapa alialikwa tena kama kiongozi wanaemuamini ingawa hana madaraka ya kiutendjai kama awali.

Barua wanayodai imeandikwa kihuni na kusainiwa na Afisa Ardhi Mteule wa Manispaa

 

Barua ya mwito wa wanakijiji 9 ambao waligomea fidia wakihitajika kuhudhuria zoezi jipya la uthaminishaji

DSCN4390 Ramani halisi ya eneo ikionesha namna upanuzi husika utakavyokuwa. Kwa mujibu wa ufafanuzi wa wananchi hao, mita 100 zinazozungumziwa zitatokana na mita 40 kuingia ndani ya eneo la mwanzo na mita 60 kutoka ndani. Lakini wanadai watumishi wa Manispaa wamegeuka makubaliano na kutaka mita 100 zipatikane zote kutoka nje.

DSCN4401 Kiwanja cha mmoja wa walalamikaji kikiwa na nyumba hizo mbili, moja ni mpya inajengwa laiki mwenyewe amedai kuandikiwa fidia ya Shs mil 1.2 tu kwa kila kitu, hatua ambayo alilalamika kuwa hawezi kujenga hata chumba kimoja mahali pengine.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO