Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA yaomba tume huru vurugu za Ndago

na Jumbe Ismailly, Singida (Tanzania Daima 18th July 2012)

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeiomba serikali iunde tume huru ya kuchunguza vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Kijiji cha Nguvumali, Kata ya Ndago, wilayani Iramba na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Ofisa wa Sera na Utafiti wa CHADEMA Makao Makuu, Waitara Mwita Mwikwabe, alisema hayo baada ya kutoka mahakamani ambako amefunguliwa shitaka la kumtolea lugha ya matusi Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM).

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa, Mwikwabe alisema endapo Jeshi la Polisi litaachiwa kuendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo, ni imani yake kwamba haki haitatetendeka kwa upande wa chama hicho.

Alifafanua kwamba dalili ambazo zimeanza kujitokeza ni kwamba siku ya tukio kabla jeshi hilo halijafanya uchunguzi wowote dhidi ya tukio hilo, walitangaza kwenye vyombo vya habari kwamba mauaji hayo yamefanywa na wafuasi wa CHADEMA.

Aidha, kiongozi huyo alisisitiza pia kwamba katika hali inayoonyesha udhaifu wa jeshi hilo kutotenda haki, licha ya kufungua jalada katika kituo kidogo cha polisi Ndago na kupewa namba NDG/RB/190/2012 na kuwataja watu 12 waliokuwa wakijihusisha na vurugu hizo, lakini hadi sasa hakuna hatua zozote zile zilizochukuliwa dhidi ya wahusika hao.

Hivi karibuni katika Kijiji cha Nguvumali, Kata ya Ndago, CHADEMA walikuwa na kibali cha kufanya mkutano wa hadhara kuhamasisha watu kujiunga na chama hicho, lakini kutokana na vurugu zilizotokea zilisababisha Mwenyekiti wa UVCCM wa Kata ya Ndago,Yohana Mpinga, kupoteza maisha baada ya kupata kipigo na kwamba jumla ya watu sita kati ya 18 waliokuwa wakishikiliwa wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO