Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeendelea na operesheni yake ya M4C kuzunguka maeneo mbalimbali ya nchi kujua mizizi ya matatizo mbalimbali yanayowakabili watanzania nchini kote, na kukiweka chama karibu zaidi na wananchi.
Safari hii ilikuwa ni zamu ya wakazi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kutembelewa na makamanda wa chama hicho hapo jana wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho Mh Godbless Lema.
Mh Lema aliambatana na viongozi na makamanda wengine wakiwemo wanachama wapya waliohamia chama hicho hivi karibuni kutokea CCM. Miongoni mwao ni pamoja na James Ole Millya, Ally Bananga na Alphonce Mawazo.
Jumla ya mikutano saba ilifanyika kwa siku ya jana, sita ikifanyika kwa kuruzu maeneo tofauti ya Simanjiro kwa kutumia helcopta na baadae kumalizia na mkutano mkubwa wa jioni katika uwanja wa shule ya msingi Mirerani iliyopo eneo la Mirerani. Lema, Mawazo na Millya ndio waliotumia chopa na wengine walitumia gari mpya za chama hicho kwa njia za barabara kutokea Arusha Mjini.
Picha zifuatazo zinaonesha taswira za matukio tofauti yaliyojiri…
Wananchi waliohudhuria mkutano wa CHADEMA eneo la Mirerani jana
Chopa inayotumiwa na CHADEMA ikijiandaa kupaa kutoka viwanja vya NMC Arusha kuelekea Simanjiro. Ndani yake wamo Mh Godbless Lema, Alphonce Mawazo na James Ole Millya.
Mwendesha baiskeli huyu alikuwa kivutio kwa wananchi na bango lake alilofunga kwenye chombo chake cha usafiri na kuzunguka nalo mitaa ya Mirerani kabla ya ugeni wa kina Millya kuwasili mjini hapo majira ya jioni jana.
Shughuli za uzinduzi wa matawi ya chama hicho katika viunga vya mji wa Mirerani. Hapa ni ofisi ya tawi la Ndesapesa. Anaezungumza na maikrofoni ni kamanda wa chama hicho na mtaalamu wa GPS
Ally Bananga aliewahi kuwa mjumbe wa kmati kuu CCM akiwakilisha vijana Arusha kabla ya kuhamia chadema akiongea na wananchi wa Mirerani kupitia vipaza sauti vya gari la matangazo wakati msafara ukielekea uwanjani kuanza mkutano wa mwisho hapo jana.
Ally Bananga akikaribishwa jukwani kuzungumza.
Sehemu ya viongozi walioketi jukwaa kuu katika mkutano huo hapo jana
James Ole Millya (alievaa rubega) akikaribishwa jukwaani na Ndg Alphonce Mawazo kuzungumza. Wote waliwahikuwa wananchama wa CCM kabla ya kuhamia CHADEMA mapema mwezi April.
James Millya akizungumza na wananchi wa Mirerani
Sehemu ya wananchi waliohdhuria wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wa CHADEMA
Mh Lema akiwajibika jukwaani hapo jana
Millya akifuatilia hotuba za wenzake kwa umakini ka anavyoonekana
Zoezi la kupokea wananchama wapya likiendelea
Magari mapya ya CHADEMA maalumu kwa shughuli za kueneza ujumbe wa vuguvugu la mbadiliko. Gari hili na mengine ndiyo yalitumiwa na waliosafiri kwa barabara kwenda Mirerani tokea Arusha mjini.
Hawa nao walilazimika kukwea juu ya mti huu ili kuweza kushuhudia kila kitu kwa uzuri zaidi
Kamera yetu iliweza kunasa taswira ya jengo la Mahakama ya Mwanzo Mirerani kama linavyoonekana pichani. Picha ya chini ni ofisi nyingine za kiserikali katika eneo hilo.
Mwananchi huyu mwanchama wa CCM, akiwa kazini jirani na eneo la mkutano nae alikuwa kivutio kwa makaamnda wa chadema hasa pale aliposimamia msimamo wake kwamba kwa namna yeyote ile hawezi kuhama CCM na kujiunga na CHADEMA. Pamoja na makelele yote lakini yeye aliweza kuendelea na kazi yake bila usumbufu.
Picha zote na Nuru Ndosi
0 maoni:
Post a Comment