Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Lema, James Ole Millya na Ally Bananga (CHADEMA) kufanya mikutano sita leo Wilayani SImanjoro wakitumia Helkopter “chopa”

Makamanda wapya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao hapo awali walikuwa viongozi wa umoja wa vijana CCM Mkoani Arusha, Nd James Ole Millya, Alphonce Mawazo na Ally Bananga wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambae awali alikuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema leo wanatarajiwa kufanya mikutano isiyopungua sita katika maeneo tofauti Wilayani Simanjiro kwa lengo la kuimarisha chama.

Mapema leo asubuhi majira ya saa tatu, makamanda hao waliondoka na chopa katika viwanja vya NMC Unga Limited Arusha kuelekea Simanjiro ambapo ilielezwa kuwa baadae jioni wataungana na viongozi wengine waliotangulia Mererani kwa usafiri wa barabara ili kufanya mkutano mkubwa maeneo hayo.

SAM_2717 Helkopta inayotumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikitua katiwa viwanja vya NMC Unga Limited Arusha mapema leo asubuhi kwa ajili ya kuwachukua viongozi hao wa chama kuelekea Simanjiro.

SAM_2743 Aliewahi kuwa diwani wa Kata ya Sombetini Jijini Arusha, Ndg Alphonce Mawazo akiwasalimia wananchi waliofika viwanjani hao mara baada ya kuingia kwenye helkopta

SAM_2754 Mh Godbless Lema (mbele), Alphonce Mawazo (mlangoni) na James Ole Millya (mwenye fimbo ya Kimasai) wakipata maelekezo ya kiusalama toka kwa rubani wao kabla ya kuanza safari ya Simanjiro kuzuru maeneo saba tofauti kusambaza ujumbe wa M4C.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO