Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mbunge (CHADEMA) ahukumiwa kifungo au kulipa faini baada ya kukutikana na hatia

 

kasulumbai Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbai (CHADEMA), na kada wa chama hicho, Robert William, wamehukumiwa kifungo cha miezi saba jela au kulipa faini ya sh 250,000 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili ya jinai.

Adhabu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Tabora, Thomas Simba, muda mfupi baada ya kumwachilia huru mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho, Suzan Kiwanga, na mwanachama mwingine, Anwaryn Kashaga.

Kasulumbai na mwenzake walifungwa pingu na kupelekwa katika mahabusu ya mahakama kitendo ambacho kililalamikiwa na wakili Mbogolo kwamba ni cha udhalilishaji na uvunjaji wa haki za binadamu.

“Unakifurahia kitendo unachokifanya? Alisikika Kasulumbai akimuuliza askari polisi aliyemvika pingu mara baada ya hukumu hiyo kutolewa.

Akisoma hukumu ya kesi hiyo, hakimu Simba alisema kuwa hii ni sawa na kesi nyingine zinazowakabili watu wengine kwamba mbunge huyo atakwenda jela miezi mitatu kwa kutoa lugha ya matusi au kulipa faini ya sh 50,000.

Pia aliwahukumu washtakiwa hao kwenda jela miezi minne au kulipa faini ya sh 100,000 baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la shambulio liletalo madhara mwilini.

Hakimu Simba vile vile aliwataka washtakiwa hao kumlipa fidia ya sh 2,000,000 mlalamikaji Fatuma Kimario, ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga.

Washtakiwa wote walilipa faini hiyo na kuachiliwa huru huku wakibaki kusubiri kulipa fidia hiyo ya sh milioni moja kila mmoja.

Awali upande wa mashtaka ulidai kuwa washtakiwa wote walitenda makosa hayo Septamba 15 mwaka jana, katika Kijiji cha Isakamaliwa wilaya ya Igunga.

Mara baada ya kuachiliwa huru, Kiwanga na Kashaga walitoka nje na kutimua mbio jambo lililowafanya watu waliokuwepo mahakamani hapo kuwashangaa.

Mapema wakili wa utetezi, Edson Mbogolo, aliiomba mahakama itoe adhabu ndogo kwa wateja wake kwa vile ni wakosaji wa mara ya kwanza na kwamba Kasulumbai (62) ana watoto 27 na wake watatu wanaomtegemea.

“Mahakama izingatie kwamba Kasulumbai ni mwakilishi wa wananchi na endapo akipewa adhabu ya kifungo, jimbo lake litakuwa wazi na hivyo litaigharimu serikali kuitisha upya uchaguzi,” alisema Mbogolo.

Makosa mengine yaliyokuwa yakiwakabili washtakiwa hao ni kumweka chini ya ulinzi isivyo halali kwa mujibu wa sheria Mkuu huyo wa Wilaya, huku kosa la nne ni wizi kutoka maungoni ambalo halikuweza kuthibitishwa na hivyo kufutwa na mahakama

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/07/mbunge-ahukumiwa-kifungo-au-kulipa-faini-baada-ya-kukutinana-na-hatia.html#ixzz21FrVxqtq

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO