Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Askari trafiki agongwa na gari Jijini Arusha na kufariki, wengine wawili wajeruhiwa vibaya

Askari mmoja wa kikoci cha usalama barabarani Jijini Arusha, koplo Augustino mwenye namba F1095 amefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya Seiani.

Tukio hilo limetokea leo maeneo ya Kibo Palace wakati askari hao wakiwa wanahojiana na dereva wa gari ndogo ya abiria eneo hilo, iliyokuwa inaendeshwa na Abdul Salum (28)

Askari waliojeruhiwa wametajwa kuwa ni Koplo Gadiel mwenye namba D 6519 na Koplo Ismail mwenye namkba F 354.

Derava aliyekuwa akiendesha gari iliyowagonga askari hao anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Blog hii inatopa pole kwa wote dugu jamaa na marafiki wa marehemu, na kuwatakia uponaji wa haraka kwa majeruhi wote. Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO