Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI DR EMANUEL NCHIMBI ATEMBELEA MAJERUHI WA BOMU KATIKA HOSPITALI YA MOUNTI MERU NA SELIANI; AKUMBANA NA ZOMEA ZOMEA ALIPOZURU ENEO LA MLIPUKO

Waziri wa Mambo ya Ndani Dr Emmanuel Nchimbi akimjulia hali mtoto huyu aliyelazwa katika hospitali ya Mt Meru baada ya kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wa Chadema jana jijini hapa.

DSC09350Awali Waziri Nchimbi akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha walizuru eneo ambalo mkutano huo ulifanyika na kutokea mlipuko lakini hawakuweza kuzungumza na mamia ya wafuasi wa Chadema walioshinda viwanjani hapo kutwa nzima wakiomboleza. Hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya wananchi hao kuanza kuimba nyimbo kama ‘parapanda italia..’ wimbo wa taifa ambao waliubadilisha maneno na kuimba “Mungu ibariki Chadema..”, tukio ambalo liliwalazimu viongozi hao kuingia kwenye magari yao na kuondoka huku wakisindikizwa na miluzi na ukunga wa ajabu.

DSC09357Kijana huyu ambae jina lake halikufahamika mara moja alijikuta akiwekwa chini ya ulinzi na wafuasi wa Chadema waliokuwa viwanja vya Soweto wakati zoezi la upimaji chanzo cha mlipuko ukiendelea, kwa kili kilichodaiwa kuwa walimtilia shaka kuwa na nia ovu eneo lile na hivyo kumkabidhisha kwa Polisi wakiomba akaguliwe.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO