Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Mh Joshua nassari akimueleza mmwenyekiti wa Chadema taifa Mh Freeman Mbowe aliyekwenda kumjulia hali alipolazwa katika hospitali ya Selian ya jijini Arusha alikolazwa mchana wa leo baada ya kupigwa sana na wananchi wanaoaminika kutoka kwa wapinzani wa Chadema katika kinyang’antyiro cha kuwania Udiwani wa Kata ya Makuyuni-Monduli uliofanyika leo.
Katika ziara hiyo hospitalini hapo, Mh Mbowe aliongozana na Mbunge wa Arusha Mjini pamoja na James ole Millya.
Aidha taarifa kutoka Makuyuni zinaeleza kuwa uchaguzi wa leo ulitawaliwa na matukio ya kushambulia watu wa Chadema wakiwemo mawakala wanaosimamia uchaguzi huo kuwakilisha Chadema, na inadaiwa kuwa kuna wakala mmoja amepigwa na kuumizwa vibaya mkono wake.
Mawakala wa Chadema walilazimika kukimbia kuacha vituo vya uchaguzi kuokoa maisha yao.
Kupigwa kwa Nassari kama wakala mkuu wa Chadema katika Kata hiyo kumeelezwa na mwenyekiti wa chama hicho kuwa kutaathiri matokeo ya uchaguzi huo hasa ya Chadema.
Blog hii ilizungumza na kiongozi mmoja wa Chadema akaieleza kuwa kwa kitendo cha wawakilishi hao wa Chadema kupigwa kunamaanisha kuwa uchaguzi huo ni batili kayika mazingira na hali halisi.
0 maoni:
Post a Comment